Kamati
ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeteua waamuzi 40
watakaochezesha Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL) inayoanza leo Mei 23 katika
vituo vinne tofauti hapa nchini.
Ligi hiyo inayoshirikisha timu
27, imegawanywa katika makundi manne ambako bingwa katika kila kundi
atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa
kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi daraja la Kwanza msimu wa
2017/18.
Timu tano zitapanda daraja hadi
Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya washindi katika vituo vyote vinne,
mshindwa bora katika vituo vya Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda
daraja kwa kuangalia vigezo vya wingi wa pointi, wastani wa mabao,
mabao kufunga na mabao ya kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa
kuwa kina timu shiriki sita.
Waamuzi walioteuliwa kuchezesha
ligi hiyo kwa kituo cha Njombe ni Elasto Msaliwa, Klement Manga, Mashaka
Lulambo, Lazaro Mbogoro, Michael Mkongwa, Alex Chitalula, Maulid
Makiwa, Michael Kilango, Edina Ndelwa na Haidal Kisingile.
Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars
ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa,
Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es
Salaam.
Kituo cha Morogoro walioteuliwa
ni Athuman Lazi, Mohammed Theophil, Seleman Kinugane, Fikiri Yusuph
‘Magari’, Nicolaus Makangara, Mwarabu Mumba, Emmanuel Muga, Herry Shao,
Shaban Juma na Makongo Katuma na timu zinazoshiriki ni Stend FC ya
Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo FC(Lindi), Muheza United ya Tanga,
Stand Misuna FC ya Singida, Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC
ya Temeke, Dar es Salaam.
Kituo cha Singida wako Meshack
Suda, Abdallah Mwinyimkuu, Sarah Bongi, Lucas Mathias, Amani Mwaipaja,
Siyachitema Kawinga, Theophil Tegamaisho, Shaaban Msangi, Aboubakar
Irume na Frederick Ndahani na timu shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi
SC (Arusha), Kitayosce FC (Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Murusagamba
FC (Kagera), Fire Stone (Manyara) na Tomato FC (Njombe).
Kituo cha Kagera walioteuliwa ni
Jonesia Rukyaa, Jamada Ahmada, Ringston Rwiza, Grayson Buchard, Grace
Wamala, Edgar Lyombo, Yahaya Juma, Adrian Karisa, Getrude Kahawa na
Ahmada Simba na timu shiriki ni Geita Town Council Fc (Geita), Gold
Sports Academy (Mwanza), Kabela City (Shinyanga), Ambassador FC
(Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa (Kigoma).
No comments:
Post a Comment