Rais Barrack Obama
amekuwa rais wa kwanza aliye mamlakani nchini Marekani kutembelea mji wa
Hiroshima tangu shambulio la nuklia wakati wa vita vya pili vya dunia.
Obama amesema kuwa kumbukumbu za tarehe 6 mwezi Agosti 1945 hazifai kusahaulika,lakini hakuomba msamaha wa shambulio hilo la Marekani ikiwa ni bomu la kwanza la kinyuklia kutumika duniani.

Takriban watu 140,000 walifariki mjini Hiroshima na wengine 74,000 siku mbili baadaye katika bomu la pili katika mji wa Nagasaki.

No comments:
Post a Comment