Shirikisho
a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe
la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama
ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagam
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga
Kutokana na ratiba ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la
Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye
michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa
mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai,
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment