
Mshambuliaji huyo aliyemaliza mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG, amelidhihirisha wazi kuihusudu klabu iliyomkuza ya Malmo FF ya nchini kwao Sweden.
Ibrahimovic, alisema angependa kuitumikia tena klabu hiyo, kutokana na mapenzi yake ya dhati kuelemea Malmo FF ambapo anapachukulia kama nyumbani kwake.
“Ninaipenda Malmö na ningependa kuitumikia hata hii leo,” alisema Zlatan
“Ninaomba radhi kwa kauli hiyo, lakini ninatarajia na kutarajia. Ila ninaomba kuweni na subra kuhusu hatma yangu.” aliongeza
Hatua hiyo imewaacha njia panda wadadisi wa soka barani Ulaya, na kuanza kuhisi huenda mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, akawa na mipango mingine tofauti ya kucheza soka lake utakapofika msimu wa 2016-17.
Meneja mpya wa Man Utd, Jose Mourinho amekua akitajwa kama kivutio kikubwa cha Ibrahimovic kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford, na ilifikia wakati walianza kuhisi huenda angekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mreno huyo.

Klabu ngingine ambazo Ibrahimovic alizitumikia baada ya kuondoka Ajax mwaka 2004 ni Juventus (2004–2006) Inter Milan (2006–2009), FC Barcelona (2009–2011), AC Milan (2010–2012) pamoja na PSG (2012-2016).
No comments:
Post a Comment