Bei ya mafuta
imepanda hadi zaidi ya dola 50 kwa pipa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka
huu mwaka 2016 wakati uzalishaji wa chini na kuongozeka kwa mahitaji ya
mafuta vikiendelea kuchangia kupanda kwa bei.

Canada ndiye muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta kwa Marekani na moto wa msituni katika mikoa iliyo magharibi, ulisababisha kupungua kwa karibu mapipa milioni moja kwa siku.
Mazungumzo ya hivi majuzi kati ya nchi za Opec na Urusi kuhusu kupunguza uzalishaji wa mafuta yamechangia kupanda kwa bei.
No comments:
Post a Comment