Muungano wa
upinzani nchini Kenya umeahirisha kwa muda maandamano ambayo umekuwa
ukiandaa kila wiki katika miji mikuu nchini humo.
Muungano huo wa Coalition for Reforms and and Democracy (CORD) umeipa serikali makataa ya siku 10 la sivyo urejelee maandamano hayo.
Viongozi wa CORD wanataka maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) wajiuzulu wakisema tume hiyo haiwezi kuandaa uchaguzi mkuu huru na wa haki mwaka ujao.
- Mwanamume afariki katika maandamano Kenya
- Odinga: Tume ya uchaguzi ni sharti ibadilishwe
Maandamano hayo yamekuwa yakikumbwa na vurugu huku polisi wakishutumiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa kutumia nguvu kupita kiasi.
Jumatatu wiki hii, mmoja wa waandamanaji alifariki kwenye maandamano mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya.
Msemaji wa serikali Eric Kiraithe Jumanne aliambia wanahabari kwamba maafisa 29 wa polisi walijeruhiwa wakati wa maandamano hayo.
Serikali hiyo imesema maandamano hayo ni haramu.
No comments:
Post a Comment