




Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Chrispino Mpinge
Serikali imewapa miezi miwili
wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo
Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha
uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha
kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar
es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote
na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo
hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za
mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa
Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao
unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa
ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya
wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na
muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda
hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na
kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo
nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la
taifa.
No comments:
Post a Comment