Wanafunzi
wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza
bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.
Makamu
wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo
ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu
ya lini fedha hizo zitatolewa.
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.
No comments:
Post a Comment