Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ndilo mbunifu na
mmiliki wa maadhimisho ya Siku ya Msanii nchini Godfrey Mngereza
(Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimbi (Katikati) na Mkurugenzi wa Kampuni
mwendeshaji wa Siku ya Msanii ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka
mwishoni mwa wiki kwenye uzinduzi wa Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka
2016 katika Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam.
Msanii
maarufu wa kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akisaini kitabu cha
wageni kabla ya kushuhudia hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya
Msanii kwa mwaka 2016. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye
Ukumbi wa Alliance Francaise ulioko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi.
Vivian Shalua (Kushoto) akifuatilia kwa makini moja ya matukio
yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla ya uzinduzi wa Matukio ya Siku ya
Msanii kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francoise mwishoni mwa
wiki. Kushoto ni Msanii wa Sanaa za Ufundi Gozbetha Rwezaula.
Marais
wa Mashirikisho manne ya Sanaa nchini kutoka kushoto Symon Mwakifamba
(Filamu), Adrian Nyamangale (Ufundi), William Chitanda maarufu kama MC
Chitanda (Sanaa za Maonesho) na Addo November (Muziki) wakifuatilia kwa
makini matukio mbalimbali ya uzinduzi wa matukio ya Siku ya Msanii mwaka
kwa mwaka 2016
Kikundi
cha Sanaa cha Safari kikitoa burudani kwenye hafla ya Uzinduzi wa
Matukio ya Siku ya Msanii kwa mwaka 2016 iliyofanyika mwishoni mwa wiki
kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment