Monday, 30 May 2016

Uganda kukata uhusiano na Korea Kaskazini

 
Museveni
Rais wa Korea Kusini amesema nchi ya Uganda imeahidi kusitisha uhusiano wake wa kijeshi na marafiki wake wa jadi Korea Kaskazini baada ya kuzuru mji mkuu wa Kampala siku ya Jumapili, chombo cha habari cha AFP kimeripoti.
 
Korea Kaskazini imetuma wakufunzi wake wa kijeshi nchini Uganda kwa miaka tisa.

 
Rais kim Jong Un wa Korea kaskazini
Nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia tangu mwaka 1963 na rais Yoweri Museveni ametembelea nchi hiyo mara tatu, AFP imeongeza.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha vikwazo vikali kuwahi kutekelezwa kwa Korea kaskazini baada ya majaribio ya nuklia ya nne mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment