Suala
la ukuaj iwa teknolojia ulimwenguni limeendelea kuthibitisha kuwa ni
suala m tambuka kutokana na kukua kwake kwa kasi ya ajabuikiwa ni pamoja na
kugusa takribani sekta zote katika ulimwengu wa leo.
Hapo awali
mtu angeweza kuelewa kwa kifupi zaidi kwamb asuala la
teknolojia pengine lingewahusu sekta ya Mawasiliano peke yake na hasa wale
ambao shughuli zao za kila siku zinategemea matumizi ya vitu kama Kopyuta na
simu hasa zile za mikononi.
Pengine katika ukanda wanchi
za dunia ya tatu wameanza kusikia suala la ukuaji wa teknolojia katika miongo ya
hivi karibuni Lakini suala hili limesikika zaidi ya
karne moja katika nchi zilizoendelea na matumizi yake yamekuwa ya kuambukiza siku
hadi siku. Suala la utandawazi limechangia kwakiasi kikubwa kuenea kwa teknolojia
mbalimbali duniani na sasa kuonekana sikitu cha nchi zilizoendelea pekeyake bali ni
kwa mataifa yote.
Hiini
kwa sababu mataifa machangayamekuwayakifanywamitajimikubwa kwa mataifa
makubwa yenyenguvu za kiuchumi duniani kutokana na utajiri wa
raslimali walizonazo.
Ujio wao katika mataifa
machanga umepelekea kuongezeka kwa kasi kwa matumizi ya teknolojia mbalimbali ili
kurahisishautendaji, usimamizi na uzalishaji katika sehemu mbalimbali za kazi.
Matumizi
kama ya vikokotoleokatikamahesabu ni teknolojiaambayoimeonekana kuwa shahidi wa
jinsi gani kazi za “gazijuto” zimewezakurahisishwa. Matumizi ya wavuti, barua
pepe, tarakilishi, nukushi na vingine vyovingi katika maofisi mbalimbali ni
ushahidi mwingine wa jinsi gani teknolojia imeendelea kushika hatamu katika s hughuli zetu
za leo.
Uwepo wa mitandao ya simu na uwezekano wa kufanya Ankara na miamala ya
kifedha ni vitu vilivyopokelewa kwa hisia hasi sana katika mataifa machanga
Lakini leotunashuhudia umuhimu wake na fikra za watumiaji zimeendelea kubadilika
na kuwa chanya juu ya uwepo wa huduma hizi na teknolojia yake.
Badala
ya kuandika barua nakuipeleka posta kisha mtumiwajia kaipokea mwezi mmoja baadaye sasa
watu wanatumia barua pepe au kuchat kwa njia ya mitandao mbalimbali na
ujumbekumfikia kila mmoja kwa muda usiozidi hata dakika moja.
Wanadamu wameendelea
kuwa wabunifu kila leo na kuja na matokeo mapya yenyetija na ufanisi wa hali ya
juu. Hakuna fan iiliyokosa teknolojia yake mpaka sasa hata kama haijafika Tanzania
Lakini ipo sehemu Fulani inatumika na watu wanafaidi.
Kampuni
ya Moovn Technologies Tanzania Limited imeingianchinina jambo jipyalenyetija na
ufanisi kwa watakaotumiateknolojiayake. Teknolojia ya Moovn inamuwezesha Mteja
kupata Usafiri bila kutoaj asho, wala haipotezi muda wakujadili gaharama zake
Kutoka ulipo mpaka pale uendapo.
Mteja
amerahisishiwa huduma na kuhakikishiwa usalama wake wakati wote. Mara tu baada ya
kuingia katika chombo cha Usafiri
gharama zitaanza kuhesabika na utakapokuwa umefika mwisho wa safari
utahitajika kuangalia simu yako ya mkononi na utakuwa umejua ni kiasi gani cha
fedha dereva wako anapaswa kulipwa kwa huduma aliyoitoa kwako.
Huduma hii imekuwanimkombozimkubwa
sana kwa dereva wa Teksi, Bajaji na Bodaboda kwani haimhitaji kuwapo kutuoni pake
kwa muda mrefubila kazi. Kwa maneno mengine teknolojia hii mpya
hapa nchini inamfanya dereva aongeze kipato chake maradufu, ilikujiunga sharti dereva
awe na simu ya kisasa “Smartphone” na anachopaswa kufanya baada ya kujiunganisha
na hudumahii ni kuhakikisha simu yake wakati wote inachaji ya kutosha kuwasiliana na wateja
wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
ya Moovn Technologies Tanzania Bw. Godwin Ndugulile akizungumza na FOFAM MEDIA amesema
tayari wamekwisha kuwasajili zaidi wa madereva 8600 wanaotumia vyombohivivya
Usafiri na kuwapa elimu ya uendeshaji na faida zake.
Bwana Ndugulile amesema teknolojia hii imefanya kazi vizuri katika mataifa
mengine ya UlayanaMarekani na sasa yeye ameona ni
vyema aileteteknolojia hii nyumbani Tanzania Kutoka
marekani kwani ameona italeta manufaa makubwa sana kwa watumiaji.
No comments:
Post a Comment