Meneja
Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiongea na baadhi ya
wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye
viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho
ya siku ya hedhi Salama mwishoni mwa wiki.
Meneja
Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiwagawia kinywaji
cha Grand Malt baadhi ya wazazi wa watoto wanaosoma katika shule
mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya TTCL Kijitonyama jijini Dar es
Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi Salama mwishoni mwa
wiki.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo wakati wa maadhimisho hayo.
Na Mwandish wetu
Meneja
Uhusiano wa nje wa kampuni ya TBL Group,Emma Oriyo, amesema kuwa jukumu
la kuwainua watoto wa kike nchini sio la serikali bali linamhusu kila
mtanzania ikiwemo makampuni,taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akiongea
wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani iliyoadhimishwa mwishoni
mwa wiki jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa siku hiyo ni muhimu
kuadhimishwa kwa kuwa inatukumbusha watanzania kutofumbia matatizo
yaliyopo kwenye jamii yetu na kuangalia namna ya kuyashughulikia.
“Hapa
Tanzania Changamoto za hedhi kwa watoto wa kike ni kubwa wengi wakiwa
wanakosa vifaa vya kuwaweka salama pia shule nyingi hazina miuondombinu
rafiki kwa wasichana kujiweka salama wanapokuwa kwenye hedhi,matokeo
yake wengi wanakuwa hawahudhuri masomo na kujikuta wamebaki nyuma ya
wenzao wa kiume”.Alisema.
Amesema
TBL Group katika miradi yake ya afya ya kusaidia jamii imeanza
kuliangalia suala hili kwa undani ili kuweza kushirikiana na wadau
wengine kukabiliana nalo “Leo kampuni yetu ni moja ya wadhamini wa tukio
hili la siku ya hedhi ambalo lengo lake kubwa ni kuelimisha jamii
umuhimu wa kuungana kuondoa changamoto na hedhi na tutaendelea na
jitihada hizi na kutekeleza miradi mingine ya kusaidia kuboresha afya
nchini”.Alisema.
Alisema
watanzania wakiungana na serikali katika kukabiliana na changamoto
hizi hali itakuwa nzuri na watoto wa kike kusoma katika mazingira
mazuri na itapelekea wafanye vizuri kwenye masomo yao sambamba na wenzao
wa kiume.
Emma
alisema kuwa hali ya kukosa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na
miundombinu isiyo rafiki mashuleni mbali na utoro mashuleni pia
inawasabishia watoto wa kike kutojiamini na wakikua bila kujiamini
wanakuwa hawawezi kutoa maamuzi sahihi.
“Wadau
wote tukiungana katika suala hili tutaweza kutekeleza dira ya maendeleo
ya taifa ambayo kwa upande wa elimu ina kauli mbiu isemayo Elimu Bora bila ubaguzi inawezekana.Timiza wajibu wako”
No comments:
Post a Comment