Maandamano ya
upinzani yanafanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupinga
uamuzi wa mahakama ya kikatiba mapema mwezi huu kwamba rais Joseph
kabila atasalia madarakani baada ya mda wake kukamilika iwapo uchaguzi
hautafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mashariki mwa mji wa Goma hali inazidi kuwa mbaya ,huku waandishi wa habari wakituma ujumbe wa Twitter kwamba jeshi limekuwa likifyatua risasi na kuwazuia raia kukongamana.
Mwandishi huru wa habari Ley Uwara alituma ujumbe wa Twitter kwa lugha ya Ufaransa kwamba hakuna uchukuzi wa umma hivyobasi watu wameshindwa kwenda kazini.

Anasema kuwa baadhi ya vijana wamekamatwa na jeshi kutumwa ili kuwasaidia maafisa wa polisi.
No comments:
Post a Comment