Na Tabu Mullah
Viongozi wa umoja na wadau wa
maendeleo wilaya mpya ya kibiti (UWAWAMAKI) mkoani Pwani umepanga
kufanya kongamano la kuunga mkono tamko la Serikali ya awamu ya Tano ya
Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuifanya Kibiti kuwa Miongoni mwa Wilaya
mpya siku ya jumapili tarehe 29 saa nne asubuhi kwenye ukumbi wa Shule
ya Sekondari TEDEO Temeke jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa Habari
leo jijini Dar es Salaam Katibu wa umoja huo Bw.Selemani Ndumbogani
amesema kuwa wanakibiti wamefarijika sana na kauli ya Serikali ya
Kuipatia Kibiti wilaya jambo ambalo lilikuwa kilio cha muda mrefu ikiwa
ni takribani zaidi ya miaka arobaini tangu uhuru na kuongezea kuwa
walikuwa mbali sana na huduma muhimu za Serikali.
Pia umoja huo umeomba wana jimbo
la kibiti hususani Rufiji kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo ili
liwe lenye mafanikio makubwa.
Miongoni mwa mambo yaliyoandaliwa
kufanywa ni pamoja na usafishaji wa mitaa,soko, maeneo ya standi ,eneo
litakalojengwa wilaya,na kuendesha dua kwa madhehebu mbalimbali ya dini
ili kuiombea kheri wilaya ya kibiti,Pia kuiombea nchi na Rais wetu wa
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli na
Mhe.Kassim Majaliwa kuishi kwa amani na usalama katika kusimamia
shughuli za Taifa.
Mwaka huu mwezi Februari Rais wa
awamu ya tano Dr.John Pombe magufuli alitangaza kuipandisha adhi wilaya
hiyo mpya ya kibiti ambapo kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa mamlaka rais ya kugawa nchi kwa kadri
ambavyo atakavyoona inafaa.
No comments:
Post a Comment