NaMwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
kimewataka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuendelea
kushirikiana ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuharakisha
maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.
Kimesema utendaji mzuri wa
viongozi hao ndani ya Baraza hilo ndiyo utakaoweza kukirahisishia kazi
Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020, hali itakayojenga
imani kwa wananchi kuirejesha tena CCM madarakati kutokana na utendaji
mzuri wa viongozi hao.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai wakati akibadilishana mawazo na Katibu
Mpya wa Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (Mnadhimu) huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
hapa.
Nd. Vuai alimpongeza kiongozi
huyo kwa kuaminiwa na Wajumbe wa Baraza hilo na kumchagua kuwa Mnadhimu
wa Wawakilishi wote wa CCM ndani ya Chombo hicho cha kutunga sheria za
nchi.
Alisema kuchaguliwa kwa Mnadhimu
huyo pamoja na msadizi wake kutasaidia kuongeza ufanisi wa kusimamia
vyema shughuli za baraza la wawakilishi ili ziende sambamba na mahitaji
ya wananchi majimboni.
Alieleza kwamba mbali na viongozi
hao kuwa na jukumu la kuandaa miswaada, kutunga sheria na kupitisha
Bajeti za nchi bado wana wajibu wa kusimamia kwa vitendo ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 pamoja na kulinda maslahi ya Chama hicho.
“Njia pekee ya kuepuka migongano
na mivutano isiyokuwa ya lazima ndani ya Baraza la Wawakilishi ni lazima
kila mara mkumbushane kufuata Kanuni na taratibu zilizopo ndani ya
Chombo chenu.
Pia nyinyi ni kioo cha Wananchi
waliokuchagueni kwa kura nyingi hivyo ni lazima muwawakilishe vyema na
kuwa mifano mizuri ndani ya jamii kwani kufanya hivyo kutaongeza hamasa
na ari ya watu wengi kuendelea kuiamini CCM.”, alisisitiza Vuai na
kuongeza kwamba Uchaguzi umekwisha na kilichobaki kwa sasa ni kila
kiongozi kufanya kazi za kuiletea nchi maendeleo endelevu.
Aidha Aliwataka Wajumbe wa
Baraza la hilo kuwa na msimamo imara na kutokubali kuondoshwa katika
Malengo kwani kuna njama na mikakati michafu inayofanywa na Viongozi wa
CUF Zanzibar wenye nia ya kuharibu Haiba ya Chama na Serikali kwa
ujumla.
“Juzi nimesoma katika baadhi ya
magazeti kwamba CUF wana mipango ya kuishtaki serikali katika Mahakama
za Kimataifa na wamezindua kitambu cha Ripoti ya Haki za Binadamu, hizo
zote ni njama za siasa zilizopitwa na wakati za kutaka kukuondosheni
katika malengo yenu na msikubali kuyumbishwa.”, alisema Vuai na kuwataka
wawakilishi wasihofu juu ya Propaganda za CUF .
Aliahidi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wote
watakapohitaji ushauri na mawazo katika shughuli mbali mbali za Chama
na Serikali .
Mapema akizungumza Katibu wa
Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar(Mnadhimu), Ali Salum Haji alisema lengo la kikao
hicho ni kujitambulisha kwa CCM na kupata nasaha, mawazo na ushauri
mbali mbali wa kiutendaji kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu huyo ili waweze
kuufanyia kazi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Salum alieleza kwamba wana nia ya
kuhakikisha ndani ya miaka mitano Bazara hilo linakuwa na mabadiliko
makubwa yatakayopelekea wajumbe wake sio tu kufanya kazi za vikao bali
wafanye utafti na kutembelea majimboni ili kubaini changamoto
zinazowakabili wananchi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Naye Katibu Mndhimu Msaidizi,
Nassor Salim Jazira, aliahidi kuzifanyia kazi nasaha na ushauri
uliotolewa na Naibu Katibu Mkuu Vuai Ali Vuai ili waweze kupiga hatua
kubwa ya maendeleo katika majimbo na Baraza hilo.
Alisema changamoto na vikwazo vya
kisiasa vinavyotengenezwa na CUF toka kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa
Marudio havitoweza kupunguza kasi ya mabadiliko ya kimaendeleo
yanayofanywa na Wajumbe wa Baraza, viongozi wa Chama na serikali kwa
uju
No comments:
Post a Comment