Yanga Yatolewa CAF
WAKATI Watanzania Tukiwa katika Hali ya
huzuni mara baada ya wawakilishi wetu katika Michuano ya kimataifa Azam
Fc na Yanga kuondoshwa katika Michuano hiyo,Hali ni Ngumu Zaidi kwa Mashabiki wa Soka nchini DRC.
Katika kile kilichoonekana kuwa kitendo
cha Mbwana Samatta kuondoka katika Klabu ya TP Mazembe kungeacha pengo
kubwa, jana hali hiyo iliweza kujidhihirisha ambapo mabingwa Hao mara
tano wa taji la Klabu Bingwa Afrika walipoweza kutemeshwa taji hilo na
Klabu ya Wydad Athletics Club ya nchini Algeria.
Hii nikutokana timu hizo mbili kumaliza
dakika 90 za mchezo huku zikiwa zimefungana goli 1-1 hali iliyoifanya
Mazembe kuvuliwa ubingwa kwa jumla la magoli 3-2 katika mechi ya awali
TP Mazembe kwa kukubali kichapo cha goli 2-1 nchini Algeria.
Kwa matokeo hayo TP Mazembe na Yanga
pamoja na timu zote zilizoishia nafasi ya 16 bora ya Michuano ha klabu
bingwa zinatarajia kupambana na timu zilizofuzu hatua ya 16 kutoka
katika michuano ya kombe la shirikisho.
Hii ikiwa na maana ya timu nane
zilizofuzu hatua hii kutoka katika michauno ya Kombe la Shirikisho
ikiwemo Esperance ya Tunisia ambayo iliifunga Azam Fc zitakutana na timu
8 Zilizofungwa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ikiwemo Yanga na
TP Mazembe
No comments:
Post a Comment