Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Katavi Eng. Abdon
Maregesi Akimuonesha athari za mvua Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia kwake) wakati akikagua daraja
la Koga lililoathirika. Daraja hilo linaunganisha mkoa wa Katavi na
Tabora.
Muonekano
wa Daraja la Koga baada ya kufanyiwa ukarabati kufuatia kuathiriwa na
mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Katavi. Daraja hilo kwa sasa
linaruhusu magari kupita ya Tani 1 hadi 3.
Muonekano
wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km 356 inayojengwa kwa
kiwango cha lami ikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CICO anayejenga barabara ya
Tabora-Koga- Mpanda yenye urefu wa Km 356, sehemu ya Tabora-Sikonge
kumaliza mradi huo kwa wakati.
Mkuu
wa Wilaya ya Sikonge Bi. Hanifa Sirengu akitoa taarifa kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya
miundombinu katika wilaya yake.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
wakati alipotembelea kiwanja cha ndege cha Tabora.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza
maelezo ya namna Vifaa vya kuongozea ndege vinavyofanya kazi kutoka kwa
mtaalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), mkoa wa Tabora.
Mkuu
wa Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa ndege wa Tabora Bw. Yahya Nassoro
akitoa maelezo ya Namna gari la kuzimia moto linavyofanya kazi katika
uwanja huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za
mwisho kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye Urefu wa Km. 356 kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya
Rais wa Awamu ya Tano aliyoitoa kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi na
Tabora.
Ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge
mkoani Tabora, mara baada ya kukagua barabara hiyo Ambapo pamoja na Mambo Mengine amesema ujenzi huo unatarajia kuanza Rasmi hivi karibuni.
‘Ujenzi wa barabara hii tumeugawa
katika sehemu tatu ili kuharakisha utekelezaji wake, Tutahakikisha
ifikapo mwisho wa mwaka huu, makandarasi wote watatu watakuwa katika
maeneo yao ya kazi’, amesema Prof. Mbarawa.
Amesisitiza kuwa wananchi
wanaostahili kulipwa fidia watalipwa kwa wakati kwa kuwa Takribani
shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Prof. Mbarawa pia amekagua daraja
la Koga linalounganisha Mkoa wa Katavi na Tabora na kuwataka viongozi wa
mikoa hiyo kuhakikisha kuwa magari yasiyozidi tani tatu ndio Yanayopita
katika daraja hilo ili kuepusha ajali hadi ukarabati mkubwa
utakapofanyika.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mlele,
Kanali Mstaafu Issa Nziku amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano kupandisha hadhi baadhi ya barabara katika Wilaya hiyo ili Zihudumiwe na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kutokana na uwezo
mdogo wa Halmashauri hiyo kuzikarabati kila wakati.
Katika Hatua nyingine Prof.
Mbarawa amekagua uwanja wa Ndege wa Tabora na kuwataka viongozi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania(TCAA) kuangalia namna bora ya ukarabati wa kiwanja hicho ili
uruhusu ndege kubwa kutua na kuongeza biashara.
Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya
siku saba ya kukagua miundombinu ya taasisi zilizo chini Ya Wizara yake
katika mikoa ya Magharibi ili kuifungua kanda hiyo kimiundombinu na
hivyo kufufua fursa za kiuchumi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri Mwakyembe aishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa viungo bandia kwa walemavu
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama
Group , Gagan Gupta wakati wa hafla ilyofanywa na kampuni hiyo ya Kamal
Steel Ltd kiwandani hapo wakati wa utoaji wa msaada wa viungo Bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh.
milioni 80, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akishukuru kampuni hiyo kwa msaada ilioutoa kwa
watanzania hao wenye ulemavu wa miguu ambapo yeye ndiye aliyewakabidhi
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akimvisha mguu wa bandia Bw. Siaga Raphael Kiboko
mara baada ya kukabidhiwa kutoka kampuni ya Kamal Steel ya jijini Dar es
salaam kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Gagan Gupta.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akizungumza na Bw. Siaga Raphael Kiboko kabla ya
kumkabidhi msaada wake wa viungo bandia vya mguu.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Gagan Gupta Ambaye ni Mwenyekiti
wa kampuni ya Kalam Steel tayari kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na Bw. Siaga Raphael Kiboko mara
baada ya kumvisha mguu wake huku Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel
Bw. Gagan Gupta pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo
wakishuhudia.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Joshua Mwamunyange mara baada ya
kumvisha mguu wakena kuanza kujaribu kutembea.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akimbidhi Bi Fatuma mguu wake wa Bandia ikiwa ni
msaada kutoka kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel ya jijini Dar
es salaam.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa kampuni ya
Kamal Steel na baadhi ya walemavu waliokabidhiwa msaada huo.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk.
Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mwenyekiti wa kampuni Ya Kamal Steel
Bw. Gagan Gupta.mara baada ya kukabidhi misaada hiyo katikati Ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta na wakuu wengine wa
vitengo kutoka kampuni hiyo.
Na Chrispino Mpinge
KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya
Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa Viungo Bandia, kwa Watu Wenye Ulemavu
16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 80.
Akifunga kambi ya kutoa viungo
bandia hivyo jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi Vifaa hivyo,
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema, serikali
itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze kukabiliana
na changamoto Zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa
bandia.
Alisema, Suala la ulemevu linagusa maisha ya kila Mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha, viungo bandia
vinauzwa kwa ghalama kubwa ambayo watu wengi wenye Ulemavu hawawezi
kumudu kununua hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake
itaendelea kutoa msaada wa vifaa hivyo.
“Jamii iamini kuwa wote ni
walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni changamoto
kubwa. Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii
muhimu Ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya
ulemavu,”alisema Dk.
Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza
kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani
Mbeya.
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama
Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa Viungo Bandia hivyo
kama Msaada, bali kama wajibu wake kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi
bandia vitawawezesha kumudu kutembea, kufanya kazi Mbalimbali Zitakazo Waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika hatua nyingine, Gupta
aliahidi kumuajiri Mmoja wa watu hao wenye Ulemavu Mwenye Taaluma ya
ufundi mitambo, Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza leo.
“Huyu atafundishwa ufundi wa
kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu Hapa, ili aweze
kusaidia kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo Ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema Gupta.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel,
Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa Mbele katika
kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa
imesaidia watu 200.
“Tutaendelea kuwasaidia kila
mara ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea Changamoto
wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki Shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
walio pokea msaada huo, Siaga Raphael, aliipongeza kampuni hiyo kwa
masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali kuwa kumbuka watu wenye Ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma ya ufundi itakazowawezesha
kujimudu kimaisha.
No comments:
Post a Comment