Nyota wa Bongo Movies Wastara Juma amesema kuwa awali baada ya kupata Ulemavu wa Maisha uliotokana na ajali ya pikipiki,alikata tamaa ya maisha.
Hata hivyo,alisema alijipa moyo akiamini hakuna linaloshindikana.
”Ulemavu huu ndiyo Ulionishawishi kuwania Ubunge Mwaka jana ili kupata Nafasi ya kutetea Haki za walemavu kwa kila hali na kuhakikisha Serikali inawasaidia kwa kuwapa huduma Nzuri za kijamii,” alisema Wastara.
Alisema kuwa bahati mbaya kura zake hazikutosha na hivyo anasubiria Uchaguzi Mkuu Mwaka 2020.
Wastara kwa sasa amefyatua filamu Mpya iitwayo ‘Faulo’ akiwa Mbioni kuachia Nyingine iyakayokwenda kwa jina la’Hapendeki’ akitumia kampuni yake Wajey film.
No comments:
Post a Comment