Monday, 4 April 2016

Wajasiriamali Dar Wanufaika na Mafunzo kuhusu fursa Mpya katika Kilimo Biashara

Margareth Nzuki - ESRF
Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akiwasilisha malengo Ya warsha kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida kufungua warsha hiyo.

Wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamefanikiwa kupata nafasi Ya mafunzo yanayohusu fursa mpya zinazopatikana katika kilimo cha biashara katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF).

Elimu ambayo wajasiriamali waliipata katika warsha hiyo ni elimu ya shamba kitalu na Ujasiriamali, elimu ya kilimo cha foda na mbogamboga, elimu ya kilimo na kufuga samaki katika matanki, elimu ya ufugaji samaki katika mabwawa, elimu ya ufugaji samaki katika Vizimba, kutazama fursa zilizopo katika ufugaji bora wa kuku na kupata elimu kuhusu Azolla ambayo inaweza kutumika kama chakula cha mifugo na pia kama mbolea.

Akizungumza katika warsha hiyo mmoja wa wawasilishaji mada, Dominic Haule alisema kilimo kina fursa nyingi lakini watu wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na kuwepo mambo mbalimbali ambayo yanayakwamisha.

Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosa elimu ya kilimo na kushindwa kupata taarifa sahihi za kiteknolojia kuhusu kilimo cha kisasa.

“Tunahitaji kutazama fursa zilizopo, zipo nyingi lakini bado tunakabiliwa na changamoto Wakulima wanakosa elimu ya kilimo kujua hata mazao bora yanakuwaje, bado kuna shida ya Pembejeo na mitaji inakuwa changamoto maana ili ufanikiwe unahitaji uwekezaji mkubwa,” alisema Haule.

Awali akitoa neno la ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida alisema Tanzania ina maeneo mazuri ya kufanyia kilimo na kinachohitajika ni wakulima kutambua njia za kufanya kilimo bora ili watakapoanza kulima waweze kupata matokeo mazuri kwa aina ya kilimo wanachofanya.

“Uchumi wa nchi Unategemea kilimo, nchi yetu ina eneo zuri la kilimo lakini bado kuna Changamoto kama mabadiliko ya hali ya nchi ni vyema kukutana na kujua njia bora za Kutumia kabla ya kuanza kufanya kilimo,” alisema Dkt. Kida.
Tausi Kida - ESRF
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya siku moja yenye lengo la kutambulisha na kuelimisha zaidi wananchi kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo zinapatikana katika sekta ya Kilimo.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Mshereheshaji katika warsha ya kutazama fursa mpya katika kilimo biashara, Abdallah Hassan.
Kilimo Biashara Workshop by ESRF
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo, Mifungo na Uvuvi , John Mapunda akielezea nafasi ya serikali kuwasaidia wajasiriamali ili kufikia malengo yao katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ESRF.

KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA

Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Hoyce Temu
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo Mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima Wakikaribishwa ukumbini na kupewa kinywaji cha K -Vant ambao walikua wadhamini wa shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Lilian Kamazima
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakifurahia kinywaji cha K-Vant.
Lilian Kamazima
Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima akakitambulishwa ukumbi kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkurugenzi wa Mwandago Investment, Chris Mwandago ambaye ni muandaji mashindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na kulia ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu.
 Fadhili Nkurlu
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akizungumza jambo.
Miss Tanzania Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akikata utepe kuzindua mashindano hayo jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (kulia), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) na Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima.
Yamoto Band
Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Miss Tanzania Arusha 2016
Wadau wa tasnia ya urembo wakifurahia jambo.
Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi h

No comments:

Post a Comment