Samson Mwigamba amejiuzulu Nafasi ya Ukatibu Mkuu ACT
Katibu Mkuu wa Chama cha siasa cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba ameng’atuka katika chama hicho kwa ajili ya kwenda masomoni.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya
Chama hicho zimeeleza kwamba Mwigamba Anakwenda kusoma Shahada ya
Udhamiri ya Biashara (MBA) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta ambapo ataanza
masomo mwezi Mei 2016.Uongozi
wa Chama cha ACT Wazalendo umeridhia maombi ya katibu huyo kwenda
kusoma Ambapo Chama kimempongeza kwa jitihada ambazo alizifanya katika
kusimika mfumo wa Chama tangu chama kianze mwaka 2014 mwezi Mei.
Aidha Chama kimempongeza Mwigamba kwa
hatua yake ya kwenda masomoni jambo ambalo litamuongezea uzoefu na uwezo
wa kuja kukitumikia chama siku za usoni.
Pia kufuatia hali hiyo Kamati ya
Uongozi imeagiza kamati ya mafunzo na uchaguzi ianze Mchakato wa kumpata
katibu mkuu mwingine wa chama hicho kwa kuzingatia katiba ya Chama
hicho.
Kwa kutambua mchango wa Mwigamba katika chama hicho ataagwa rasmi April 25 ili kumtakia masomo mema.
No comments:
Post a Comment