Waziri
Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amerejea Nchini
Kenya Baada ya kumaliza Mapumziko yake ya Siku tatu huko Lubambangwe
katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita, Alikomtembelea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyepo Mapumzikoni.
Akizungumza katika Uwanja wa Michezo wa Shule ya Sekondari ya Chato kabla ya kuruka kwa Helkopta, Mheshimiwa Odinga amemshukuru rafiki yake Rais Magufuli kwa kumpokea na pia amewashukuru Wananchi wa Chato kwa ukarimu wao kwa wageni.
Mheshimiwa
Odinga pia amesema ana imani kuwa Rais Magufuli ataisaidia Tanzania
kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini Unawakabili
wananchi wake.
"Lakini
mimi najua yeye Mwenyewe ana maono, anaona mbele na anajua yale ambayo
yanatakiwa yafanyike ili Tanzania iinuke, itoke katika hali ya Ufukara
na kuwa katika hali ya maendeleo zaidi" Amesema Mheshimiwa Odinga.
Mheshimiwa
Raila Amolo Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga waliwasili Chato Tarehe 02
April, 2016 kwa Mapumziko na kuisalimia Familia ya Rais Magufuli ambayo
ni familia Rafiki.
Katika
Hatua nyingine Rais Magufuli ameahidi kutoa madawati na vitabu kwa
wanafunzi wa shule tatu za Msingi zilizopo Chato, ambao walijitokeza katika uwanja wa Sekondari wa Chato, wakati Rais Magufuli akimuaga Mgeni
wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga.
Shule hizo ni Chato, Kalema na Kitela.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016
No comments:
Post a Comment