Thursday, 21 April 2016

Naibu Meya amepatikana Kupitia Chama Cha CUF Mussa Swedi Kaffana


Mussa Swedi- naibu meyaMachi 22, Mwaka huu alipatikana Meya wa Jiji la Dar e salaam Isaya Mwita (CHADEMA) kupitia Vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA , baada ya  kuishinda CCM iliyopata kura 67, huku UKAWA wakipata kura 84, ambapo kura 7 zili haribika, ambapo Nafasi ya Naibu Meya wa Jiji hilo ilibaki wazi.

Mapema leo zoezi la Uchaguzi wa kumpata Naibu jiji la Dar es salaam, ambapo katika Uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Mussa Swedi Kaffana (Diwani wa CUF kata Ya Kiwalani) ametangazwa mshindi wa nafasi ya unaibu Meya wa Jiji hilo baada ya kuchaguliwa kwa kura 10, dhidi ya Mpinzani wake Mariam Burida (CCM) kuambulia kura 6, Na wala hakuna iliyoharibika.

No comments:

Post a Comment