CUF:Serikali inaua Uhuru wa Vyombo vya Habari na Kuwanyima Wananchi kupata Haki yao ya Kuhabarishwa
Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi CUF Abdul Kambaya.
Na Chrispino Mpinge
Hakuna asiye fahamu Umuhimu wa vyombo
vya Habari katika Jamii kwani vinamchango Mkubwa katika maendeleo ya
taifa, majuma kadhaa yaliyopita waziri mwenye Dhamana ya kusimamia
tasnia ya habari nchini Nape Nnauye alitangaza Mabadiliko katika
urushwaji wa Matangazo ya bunge kupitia Luninga ya Taifa TBC, ambapo
alisema halitakuwa la moja kwa Moja kutokana na Gharama za Uendeshaji.
Je kuna Umuhimu wowote wa kurusha Matangazo ya Bunge moja kwa moja?, jibu la swali Hilo Analo Mkurugenzi
wa Habari na Uenezi wa Chama cha Wananchi CUF Abdul Kambaya, Ambapo
katika Mkutano wake na Waandishi, leo Jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa Bunge likirushwa moja kwa moja linaongeza uwajibikaji, uwazi hivyo
kutolionesha moja kwa moja ni kinyume na sheria ya Uhuru wa Habari
kifungu cha 18 katiba ya mwaka 1977.
Naibu Mkurugenzi huyo amesikitishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvinyima uhuru vyombo
binafsi vya habari katika kuripoti habari za bunge kwani amesema kuwa
Bunge limeanzisha kituo chake cha kurusha matangazo ambapo wanahabari
watakuwa Wanapatiwa habari na chombo hicho, pia hairuhusiwi kwa
muandishi kuingia na kamera au kinasa sauti bungeni jambo ambalo
amelifananisha na udikteta.
Kutokana na hayo Naibu Mkurugenzi wa
Habari Kambaya amesema kuwa chama chake cha CUF kipo tayari kushirikiana
na vyombo vya habari binafsi kupambana kufanikisha kuwa Uhuru wa vyombo
vya habari unapatikana kwani gharama za uendeshaji sio sababu ya msingi Akidai kuwa luninga ya Taifa inapata ruzuku ya serikali inayo tokana na
kodi za wananchi, Hivyo isiwe kisingizio cha kuwaficha wananchi ili
madudu ya serikali yapite bila kupingwa.
No comments:
Post a Comment