Friday, 22 April 2016

Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi Kutoa Millioni 50 kila kijiji


Serikali imesema kuwa baraza la uwezeshaji Wananchi(NEEC),limeanza kutengeneza taratibu Wa namna ya fedha Milioni 50 kwa kila kijiji Zitakavyoweza kuwafaisha Wananchi wote Vijijini Wakiwemo Vijana na Wanawake.

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa nchini Sera, Uratibu na Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Muhagama, amesema fedha hizo zitatolewa kwa kila Mtanzania bila kujali itikadi ya Vyama kama habari ambazo zinasaambaa sasa kuwa Watagawiwa Wanachama wa CCM, pekee.Waziri Muhagama, amesema jambo hilo linalozungumzwa ni hofu tu ya baadhi ya watu na kuongeza kuwa serikali itazingatia utaratibu Wa kisheria wa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia Watanzania wote wanaohusika na Mpanngo huo.

Mhe. Muhagama amesema kuwa fedha hizo zilikuwa ni ahadi ya rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kampeni zake ambazo zipo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini haimaanishi kuwa fedha hizo zitagawiwa kwa wanachama wa chama hicho Pekee.


No comments:

Post a Comment