Malawi
na Nigeria zimekutana kwenye collabo moja ya nguvu. Supastaa wa rap
kutoka Malawi, Tay Grin ameachia single mpya aliyoipa jina, Chipapapa na
kumshirikisha nguli wa Muziki wa Nigeria, 2 Face Idibia aka 2 Baba.
Ngoma hii kali na ya kuchezeka, imetokana na urafiki wa muda mrefu kati ya wasanii hawa.
“Nimemfahamu
2 Baba kwa miaka mingi na tumekuwa tukiongea siku zote kuhusu kolabo.
Ni Msanii mwenye kipaji kikubwa na kufanya kazi naye ni furaha kubwa
kwangu,” anasema Tay.
Akiutambulisha
Chipapapa kwa wapenzi wa muziki Afrika Mashariki, Tay ametoa ujumbe Huu
kwao: Nikijitambulisha tena kwa Afrika Mashariki, ningependa
kuwashukuru mashabiki Wangu wa kitambo kwa kuniunga mkono pamoja na
muziki wangu. Kwa mashabiki wangu Wapya, salamu za pekee kutoka Malawi
kwenu nyote. Nina hamu kubwa ya kuja kwenu na Kuwaburudisha.”
Video
ya Chipapapa ilifanyika Afrika Kusini kwenye mji wa machimbo ya madini
wa Nigel na kuongozwa na Bruce Patterson. Ni video inayoonesha uzuri wa
Afrika kwa kutumia uchezaji, Rangi na watu wazuri waliovaa nguo
mbalimbali za Kiafrika.
Tay
Grin amechukua Mchezo wa kizamani wa Kimalawi na kuuweka katika wimbo.
Chipapapa ni mchezo ambao wengi waliufarahia enzi wakiwa watoto.
“Ni
mchezo Unaotukumbusha wengi wetu katika muda fulani wa ujana wetu,”
amesema Tay na kuongeza, “2 Baba kisha alilielewa wazo na kwa haraka
akaongeza Michezo mingine Waliyonayo Nigeria.”
Tay
Grin ana orodha kubwa ya kolabo alizowahi kufanya ukiwemo wimbo ‘Nyau’ Aliomshirikisha Mshindi wa Tuzo za MTV, Nameless wa Kenya.
Muziki
wa Grin unawalenga vijana na kuwataka wajivunie nchi zao na utamaduni
wao. Kuwajibika, kutumia vipawa walivyopewa na Mungu na kutafuta thamani
katika kuchangia Mustakabali mzuri. Pia kusisitiza hitaji la kuondoa
mambo hasi na kutojikatia tamaa.
Akianza
kufanya rap tangu akiwa mdogo, Tay alivutiwa na wasanii wakongwe kama
Jay Z, KRS 1, B.I.G na Tupac. Ili kupata aina yake tofauti ya rap, Tay
aliangalia ladha za Kiafrika na Utamaduni wa Malawi kumsaidia
kutengeneza mtindo wake wa pekee.
Tay amewahi kutumbuiza kwenye shindano la Big Brother Africa (2007/2008).
No comments:
Post a Comment