Dar es Salaam. Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya The Foundation
for Civil Society (FCS), imetenga Sh 300 milioni kwa ajili ya
kugharamia elimu ya uchaguzi mkuu kwa watu wenye ulemavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga
aliliambia gazeti hili jana kuwa fedha hizo zitagawiwa kwa asasi za watu
wenye ulemavu zilizosajiliwa tu.
“ Ushiriki wa watu wenye ulemavu katika michakato
ya kidemokrasia mara nyingi umekuwa hafifu kutokana na sababu
mbalimbali, ikiwamo hali yao ambayo baadhi huwawia vigumu kufika hata
kwenye vituo vya kupigia kura,” alisema Kiwanga.
Alisema, pia kuna tatizo la upatikanaji wa taarifa
za msingi zinazohusu mchakato wa Kura ya Maoni na uchaguzi. Hii
inatokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya kundi hilo la watu wenye
ulemavu, alisema.
Hii si mara ya kwanza
Alisema kuwa hii ni mara ya pili taasisi hiyo
kutoa fedha za kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu. Awali tulifanya
hivyo wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010, alisema. Alifafanua kuwa
ruzuku ya 2010, ilitolewa baada ya asasi hizo kubainisha changamoto
zinazowakabili watu wenye ulemavu kuelekea kwenye uchaguzi huo.
“FCS tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na watu
wenye ulemavu na sasa tunaamini hatua hiyo ya kuwasaidia katika
upatikanaji wa elimu, itawawezesha kushiriki kikamilifu katika uchaguzi
huo unaopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” alisema.
Kiwanga alitaja baadhi ya matatizo yanayowakabili
watu wenye ulemavu nyakati za chaguzi kuwa ni pamoja na kukosekana kwa
watafsiri wa lugha za alama wakati wa kampeni na hata katika vituo vya
kupigia kura.
Alieleza kuwa taasisi hizo za kiraia bara na
visiwani, zinatakiwa kutuma maombi ili kupata fedha hizo zinazotolewa
kama ruzuku kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
“Watu wenye ulemavu wana haki ya kuchagua na
kuchaguliwa, hivyo tunatoa ruzuku hiyo ili kuziwezesha asasi zao
kuendesha mafunzo na kuwashawishi watu wenye uwezo wajitokeze, watambue
haki yao ya kikatiba na kugombea nafasi mbalimbali.
Pia tunawataka wadau kuandaa mazingira mazuri kwa
watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kushiriki uchaguzi huo kikamilifu.,”
alisema.
Alisema FCS inatoa ruzuku hiyo kama sehemu ya
wajibu wake katika kuhakikisha kuwa jamii ya watu wenye ulemavu nayo
inashiriki uchaguzi mkuu katika hatua zote; kujiandikisha kwenye Daftari
la Kuduma la wapigakura, kugombea, kuchagua na kuchaguliwukumu lake la kuhakikisha kwamba asasi za kiraia zinakuwa chachu kwenye
mchakato wa maendeleo, wenye kulenga kuleta mabadiliko kwa wananchi na
kuwawezesha kutambua utekelezaji wa sera, utawala bora na uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment