Mashabiki ya timu ya Yanga.
WANACHAMA wa Yanga kila mmoja anatakiwa kuchangia Sh250 kila
wiki sawa na Sh200 milioni kwa mwaka ili kufanikisha ujenzi wa Uwanja wa
kisasa wa Kaunda, jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo
uliofanyika kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay Dar es Salaam,
uongozi wa Yanga uliwahakikishia wanachama wa klabu hiyo kuwa ujenzi wa
Uwanja wa Kaunda unaanza mwezi Juni kama ulivyopangwa na sasa
kinachotakiwa ni kupatikana kwa Sh32 bilioni.
Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga, tayari
wameshafanya mazungumzo na Kampuni ya Unit Trust of Tanzania ambao ni
wataalamu wa kiuchumi wenye uwezo wa kufanya mipango ya upatikanaji wa
fedha kupitia benki na taasisi za kifedha na kwamba hadi mwezi Mei fedha
hizo zitakuwa zimeshapatikana.
Uongozi huo pia uliwataka wanachama wa Yanga kila
mmoja kuchangia Sh250 kila wiki kwa lengo la kupata Sh8 bilioni kutoka
katika vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwamo makusanyo ya ada za
uanachama, michango mbalimbali, harambee, Kalenda na mauzo ya jezi na
bidhaa zenye nembo ya Yanga ili kuwezesha kukamilika kwa ujenzi wa
uwanja huo.
Katika hatua nyingine Makamu mwenyekiti wa Yanga,
Clement Sanga alitangaza kuwavua rasmi uanachama aliyekuwa katibu mkuu
wa klabu hiyo, Celestine Mwesigwa na msemaji wa klabu hiyo, Louis
Sendeu pamoja na mwanasheria Godwin anayemiliki Kampuni ya Auda &
Company Advocates kwa kile alichoeleza kuwa wamekiuka katiba ya Yanga
kwa kuishtaki klabu hiyo wakati wao ni wanachama.
Mwesigwa ameishtaki Yanga kwa kuwa anaidai Sh183.4
milioni, wakati Sendeu anadai Sh79.9 milioni huku mwanasheria Godwin
anadai Sh4.5 milioni baada ya kupewa jukumu la kushughulikia kesi ya
Steven Marashi na Wisdom Ndlovu.
Mbali na hilo pia Sanga alisema kamati yake ya
utendaji imeamua kufuta posho zote zilizokuwa zikitolewa kwa wajumbe wa
Kamati ya utendaji ya Yanga.
KATIBA YAGOMA
Wanachama wa Yanga jana waligomea kufanya marekebisho ya katiba ya kupitisha kipengele cha kumchagua mwenyekiti na makamu, iwapo wanamaliza muda wao basi wachague viongozi wengine wawapendao kuwarithi.
Wanachama wa Yanga jana waligomea kufanya marekebisho ya katiba ya kupitisha kipengele cha kumchagua mwenyekiti na makamu, iwapo wanamaliza muda wao basi wachague viongozi wengine wawapendao kuwarithi.
Hoja hiyo ilipingwa vikali kwa madai kuwa hawataki
kuburuzwa katika hilo na badala yake waachiwe uhuru wao wa kuchagua
kiongozi wanayemtaka kama ilivyo sasa.
Kipengele hicho cha tano kilichowasilishwa na
uongozi wa Yanga cha marekebisho ya katiba katika uchaguzi wa viongozi
wa Yanga kilisema kutakuwa na uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti ambao watakuwa na tiketi moja na pamoja waunde kamati ya
utendaji yenye nguvu ya kuajiri na kufukuza pale inapohitajika.
Pia kipengele hicho kilisema mwenyekiti na makamu
wachague Kamati ya utendaji wanayoitaka wao kwa sababu Kamati ya
utendaji iliyopo hivi sasa iliyochaguliwa na wanachama, baadhi ya
wajumbe wanaonekana siyo waaminifu, ambapo wanachama waliridhia uamuzi
huo.
“Naombeni ridhaa yenu ya kuchagua kamati ya
utendaji ninayoitaka, hii niliyonayo naona wengine siyo waaminifu na
wamekuwa wakiutukana uongozi,” alisema kiongozi mmoja wa Yanga.
Uongozi wa Yanga pia uliwasikilizisha ‘tape’ wanachama wa klabu
hiyo ambayo ilisikika sauti ya mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji
ambaye aliwatukana na kuwadhihaki viongozi wenzake kutokana na ziara yao
ya Uturuki kwa madai kuwa haikuwa na faida.
Ombi hilo lilipokelewa na wanachama wa Yanga na kutaka kiongozi huyo achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye kamati hiyo.
Ombi hilo lilipokelewa na wanachama wa Yanga na kutaka kiongozi huyo achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwenye kamati hiyo.
Wakati huohuo; Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utawala Bora, Kapteni mstaafu George Mkuchika ameteuliwa kuunda bodi ya
udhamini ya Yanga.
No comments:
Post a Comment