Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad,amefika katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini dar es salaam kufuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim lipumba na wafuasi 29 wa chama hicho wanaotuhumiwa kutenda makosa matatu,ikiwamo kufanya mkusanyiko na maandamano, kinyume cha sheria.
Maalim Seif, ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya
Mapinduzi Zanzibar SMZ amelakiwa na Prof. Lipumba na mamia wa wafuasi wa
chama hicho waliofika katika mahakama hiyo kufuatilia kesi hiyo pamoja
na kuwadhamini wafuasi wenzao.
Wakili wa upande wa jamhuri, amewasomea mashtaka washtakiwa wawili
kati ya 30, ambao ni Shhaweji Mketo na Hemed Abdallah, ambapo
wanakabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kufanya mkusanyiko usio
halali na maandamano, kinyume cha sheria.
Mashtaka mengine, wanayotuhumiwa nayo ni kula njama kwa nia ya
kutenda kosa na kufanya fujo, kinyume cha tamko la polisi lililowazuia
kukusanyika na kuandamana.
Wanatuhumiwa kutenda makosa hayo maeneo ya mbagala, jijini dar es
salaam ambapo wote walikana makosa hayo na wako nje kwa dhamana hadi mei
6, mwaka huu kesi yao itakapokuja kwa ajili ya usikilizaji wa awali.
Watuhumiwa wengine 20 pia walipata dhamana baada ya kukamilisha
masharti ya dhamana na usikilizaji wa awali wa kesi yao utafanyika mei
6, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, maalim Seif
aliwashukuru wafuasi wa chama chake, kujitokeza kwa wingi na
waliowadhamini watuhumiwa akisema hiyo inaashiria kuwa tatizo
linalowakabili wenzao siyo lao peke yao, bali ni la wote.
No comments:
Post a Comment