Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema uharibifu wa
mazingira katika nchi zinazoendelea ni kati ya sababu zinazofanya nchi
hizo ziendelee kuwa maskini.
Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk.
Binilith Mahenge, alisema pamoja na jitihada za kukabiliana na uharibifu
wa mazingira, hali imeendelea kutoridhisha na kuwa takribani hekta
400,000 za misitu zinapotea kila mwaka huku takwimu za uchomaji moto
ovyo kwa kipindi cha mwaka 2000 hadi 2011 kumekuwa na matukio 1,123,000
katika mikoa ya Rukwa, Kigoma, Tabora, Mbeya,
Dk. Bilal aliyasema hayo jana, jijini Dar es Salaam, wakati wa
uzinduzi wa ripoti ya pili ya hali ya mazingira nchini nchini ya mwaka
2004, iliyoandaliwa na Wizara ya Mazingira.
Alisema upo uhusiano mkubwa kati ya mazingira na umskini kwa maana
ya kwamba uharibifu wa mazingira unachangia kuongezeka kwa umaskini na
kwamba kadri hali ya umaskini inavyoongezeka inasababisha uharibifu wa
mazingira.
“Kwa maana hiyo umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira nchini
unachochewa zaidi na ukweli kwamba mazingira ni mhimili wa sekta za
uzalishaji kama vile kilimo, utalii, uvuvi na madini,” alisema na
kuongeza:
“Changamoto iliyopo ni kuhakikisha mazingira na maliasili zetu
zinatumika katika njia endelevu kwa kuzingatia uwiano mzuri kati ya
matumizi ya maliasili, hifadhi zake na uwezo wake kuendelea kutoa huduma
tunazozipata.”
Dk. Bilal alisema ili kusimamia masuala ya hifadhi ya mazingira kwa
ufanisi ni lazima kudhibiti shughuli za binadamu zinazoathiri
mazingira, masuala ya kijamii na kiuchumi kama vile ongezeko la watu,
shughuli za kiuchumi zinazoendana na matumizi yasiyoendelevu ya
mazingira zinazoweka shinikizo kubwa katika mazingira na kusababisha
uharibifu.
Aidha, Makamu wa Rais alizitaka mamlaka za usimamizi kuhakikisha
sheria, kanuni, mipango na programu mbalimbali zinazoandaliwa
zinasimamiwa na kufuatiliwa kwa juhudi zote.
No comments:
Post a Comment