Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya milipuko 30 inayodaiwa kukamatwa baada ya polisi kuwakamata watu 10 katika eneo la Kidatu, mkoani humo
Morogoro. Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada
ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera
nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa
nchini Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa
polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana
(Aprili 14 mwaka huu) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha
Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata
taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa
kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua
kufatilia nyendo zao.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba
uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza
kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka,”
Alisema polisi waliendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni.
No comments:
Post a Comment