Monday, 5 June 2017

Yaliojiri leo Ikulu jijini Dar es salaam

unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimu Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
 
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe kutoka kwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mjumbe Maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Leonard  She Okitunda na ujumbe wake na wa Tanzania alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia malori mawili ya kuzolea taka baada ya kumaliza mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipofika kumtembelea na kukabidhi msaada wa magari hayo Ikulu jijini Dar es salaam  leo Juni 5, 2017MAZU01
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kuwasilisha ujumbe huo leo Juni 5, 2017
4
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017
MAZU1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe walioongozana na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017
MAZU2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana baada ya  mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017
MAZU3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana baada ya  mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Msumbiji na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Jenerali  Atanasio Salvador Ntumuke alipofika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi ujumbe maalumu leo Juni 5, 2017
PICHA NA IKULU

Madrid walivyosherekea kutwaa kombe la mabingwa Ulaya

 Real Madrid sasa ina makombe 12 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku mchezaji wake Cristiano Ronaldo akiwa amefikisha manne.
Ronaldo, wachezaji wa Madrid, benchi la ufundi linaloongozwa na Zinedine Zidane, usiku wa kuamkia leo wamekutana kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid na kufanya sherehe kubwa ya kufurahia ubingwa huo.
Kila upande umekuwa na furaha hasa baada ya ubingwa huo ambao ulionekana ni mgumu kwao.



Balozi Cisco Mtiro amefariki dunia

Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan  jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Cisco Mtiro alikuwa Balozi wa Tanzania nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia, Singapore na Laos.
Kwa mujibu wa familia yake, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B jijini Dar es salaam ambapo Taratibu za mazishi zinaendelea

Kongamano la Kitaifa la Mazingira

unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kufunga Kongamano la Kitaifa la Mazingira lililofanyika kwenye ukumbi wa kanisa Katoliki, Mwitongo Butiama.
1
Mama Maria Nyerere akichangia maoni yake wakati wa kufunga Kongamano la Taifa la Mazingira lililofanyika Mwitongo Butiama kwenye kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa imeadhimishwa Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Vijana Wampongeza Rais Magufuli kwa Ulinzi wa Rasilimali.

Image result for magufuli
Na Jonas Kamaleki -MAELEZO
Vijana Wazalendo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizozichukua kuwapinga wanyonyaji wa uchumi na rasilimali za nchi kupitia sekta ya Nishati na Madini.
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo Tanzania, Bwana Mwita Nyarukururu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Bwana Mwita amesema ana hakika kuwa Watanzania wanafuatilia juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika sekta ya Nishati na Madini kwa kuunda Tume ya wataalam mbalimbali kufanya uchunguzi na upembuzi yakinifu katika madini.
“Wote tumeshuhudia ripoti ya wataalam wa madini chini ya Mwenyekiti, Prof. Abdulkadir Mruma ambapo Tume imeeleza masikitiko yake makubwa dhidi ya makampuni ya madini nchini yanavyokwapua na kusafirisha raslimali zetu bila Taifa kunufaika”, alisema Mwita
Aidha, Mwita amesema kuwa unyonyaji na uhujumu uchumi katika sekta ya madini umekuwa ukipigiwa kelele kwa takriban miaka 17 na wazee pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya tahadhari yao kwa Taifa kuwekeza katika uzalishaji wa madini kutokana na mikataba kuwa ya siri na mibovu isiyonufaisha wananchi.
Aidha wamemwomba Mhe. Rais kuvunja mikataba ambayo haina maslahi kwa taifa bila kujali udogo au ukubwa wa kampuni hizo, ikiwa ni pamoja na kupeleka Bungeni mikataba na sheria zote zinazohusu nishati na madini kwa lengo la kujadiliwa upya kwa maslahi mapana ya Taifa .
Kwa upande wake, mjumbe wa Jukwaa la Wazalendo, Bi. Rose Manumba amesema inashangaza kuona huduma za kijamii kama sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu zinazorota kwa kukosa fedha wakati matrililioni ya fedha yanachukuliwa na wajanja wachache.
Amemuomba Mhe. Rais na wananchi kwa ujumla wasichoke katika mapambano haya ya kukomesha wizi wa raslimali za Watanzania walizopewa na Mungu.
“Kwa kweli tumuunge mkono Mheshimiwa Rais katika vita hii ili nchi yetu na raslimali zake ziwe na manufaa kwa kizazi chetu na vizazi vijavyo”, alisema Manumba.
Mwezi uliopita Mhe. Rais alipokea Ripoti ya uchunguzi wa Makinikila ambayo ilionyesha kuwa tani za dhahabu na madini mengine yenye thamani kubwa yalipatikana kwenye mchanga uliokuwa usafirishwe nje ya nchi. Katika ripoti hiyo jumla ya takriban tani 15 za madini zilikutwa kwenye makontena 277 ya makinikila yayozuiliwa kusafirishwa nje na Mhe. Rais Magufuli, thamani yake inakadiriwa kuwa ni shilingi za Kitanzania trililioni 1.3.
Kufuatia ripoti hiyo, uteuzi wa Waziri mwenye dhamna ya Nishati na Madini, Prof. Sospiter Muhongo ulitenguliwa na Mhe. Rais, na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Madini Nchini, alisimamishwa kazi.

Juventus walivyorejea

 Baada ya kupoteza kwa kufungwa kwa mabao 4-1 dhidi ya Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Juventus wamerejea nyumbani Italia.
Pamoja na kuukosa ubingwa, mashabiki walionekana kuwapongeza wakiwapungia mkono kuonyesha bado wanawapa heshima kubwa.








Islamic State yakiri kufanya shambulio London

Polisi wa kupambana ugaidi London
Polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao hamsini walijeruhiwa .
Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.
Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.
Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.
Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari


Sunday, 4 June 2017

ZILIZOPEWA KIPAUMBELE NA WAHARIRI WA MAGAZETI KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETINI LEO JUMATATU JUNI 05 2017




Lowassa:yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya yana matatizo Rais Magufuli

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli alianza vizuri kwani yapo mambo aliyoyafanya ni mazuri lakini pia yapo mambo mengine amefanya yana matatizo.
Lowassa amesema haya alipokuwa akifanya mahojiano na kusema kwa sasa tumuache Rais Magufuli aendelee na kazi yake lakini baadaye ndiyo watu waweze kumuhukumu kutokana na mambo ambayo ameyafanya.

Mwanafunzi wa ajali ya Lucky Vincent afya yake yaimarika


Mtoto Doreen Mshana, manusura wa ajali ya Lucky Vincent, ameruhusiwa kutoka Hospitali na sasa ameungana na wenzake wawili katika nyumba maalum wanamoishi, Marekani, jimbo la Iowa.
 Awali, wanafunzi wengine waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy Hospital, Sioux City, Saidia Awadh na Wilson Tarimo,   waliruhusiwa kutoka hospitali walimokuwa wakitibiwa.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa sasa Doreen, ameungana na wenzake baada ya hali yake kuimarika.
 Doreen, alibaki hospitali hapo kutokana na majereha makubwa aliyopata na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo.

Cristiano Ronaldo mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

Cristiano Ronaldo ameithibitishia dunia yeye ni mchezaji wa aina yake baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitano mfululizo.
Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiitwanga Juventus kwa mabao 4-1 na kube ubingwa wa Ulaya.
Mabao hayo mawili yamemfanya amfikie na kumvuka mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona ambaye alikuwa na mabao 11.

Saturday, 3 June 2017

ZILIZOTAWALA KATIKA KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 04 2017




kuadhimisha siku Mazingira Duniani

bund1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akitoa maelezo ya awali ya ufunguzi katika mijadala ya kuadhimisha siku Mazingira Duniani Wilayani Butiama Mkoni Mara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”
bund2
Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Mjadala unaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
bund3
Mjadala ukiendelelea pichani, Wanajopo wa mada ya kwanza ya “Tanzania Bila Mkaa na Kuni Inawezekana?” kutoka kushoto ni Ndugu Charles Meshack Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo Mkurugenzi Mkuu, wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Maria Sarungi (Mwendesha Mada) na Eng. Estomih Sawe Mkurugenzi Mtendaji TaTEDO (Center for Sustainable Modern Energy Initiative in Tanzania). Kongamano linaendelea Butiama katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
bund4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba akifuatilia mjadala katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Butiama- Mara. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Mijadala mbalimbali inaendelea katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mahusiano Endelevu Kati ya Binadamu na Mazingira.”

Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu ‘Ngosha’ Wasafirishwa Mwanza leo

KANYA1
Baadhi ya wawakilishi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiaga mwili wa marehemu Francis Maige Kanyasu (86) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo. Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo na wakati akiendelea na matibabu mauti yakamkuta.
KANYA2
Mwili wa marehemu ukiwa umebebwa tayari kwa safari ya kuelekea Misungwi mkoani Mwanza ambako mazishi yatafanyika.
KANYA3
Baadhi ya wafanyakazi wa Muhimbili wakisubiri kuuaga mwili huo leo. Kulia ni Zuhura Mawona ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi.
KANYA4
Baadhi ya watu waliofika wakiuaga mwili huo leo.
KANYA5
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Marcel Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulusubisya akizungumza kabla ya shughuli za kuaga mwili huo leo.
KANYA6
Baadhi ya watu waliofika kuaga mwili huo leo.
KANYA7
Mkurugenzi wa Huduma na Upasuaji wa Muhimbili, Dk Julieth Magandi akiwashukuru watu mbalimbali walofika kuuaga mwili huo leo.
KANYA8
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dk Juma Mfinanga akieleza jinsi Hospitali ya Muhimbili ilivyokuwa ikimpatia matibabu mzee Francis Maige Kanyasu.
KANYA9

Mwili wa marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu  umeagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  na kusafirishwa na serikali kwenda kijijini kwao Igokero wilayani Misungwi.
Shughuli ya kuuaga mwili huo imeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamaii , Jinsia , Wazee na Watoto, Marcel  Katemba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Mpoki Ulusubisya.
Akizungumza katika shughuli hiyo Bwana Katemba ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa walizofanya za kumpatia tiba na kumuhudumia kwa kipindi alichokuwa amelazwa  hospitalini hapo.
“Nawapongeza Muhimbili kwa juhudi zenu ni kweli mlitaka kuokoa maisha ya mzee wetu, lakini kazi ya Mungu haina makosa , pia sina budi kuwashukuru majirani zake na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Malapa kwa kujitoa naomba mfanye hivyo hata kwa wazee wengine’’ amesema Katemba.
Naye Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk. Juma Mfinanga amesema walimpokea Mzee Kanyasu Mei 25, 2017 akitokea Hospitali ya Amana alikokua akipatiwa matibabu na walipomfanyia vipimo vya awali waligundua kwamba ana maradhI ya Kifua Kikuu ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu kutokana na mazingira aliyokua akiishi.
Hivyo Dk. Juma ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kwenda hospitalini mapema pindi mtu anapoona hali yake ya kiafya si nzuri kwani ukiwahi hospitali ni rahisi kupata  tiba na kupona kuliko kusubiri hadi ugonjwa uwe sugu.

Mavunde azindua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi jijini Mwanza

index
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia kazi, jira na maendeleo ya Vijana amefungua mpango wa mafunzo ya ufundi wa kisasa wa kutengeneza viatu kwa njia za kisasa kwa vijana 1000 wanaotaka mikoa zaidi ya kumi nchini.
Akizundua mpango huo, Mhe Mavunde, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wa kujiajiri vijana na pia kutumia bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo kwa ajili ya kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi nchini.
Amesema, serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha inatekeleza azma ya ujenzi wa viwanda kwa kuwajengea uwezo vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa katika kujiandaa na mfumo wa mapinduzi ya viwanda ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.
Aidha amewataka vijana kutochagua kazi au kubweteka kuwa kazi rasmi ni zile za ajira ya moja kwa moja serikali au sekta binafsi, amewataka vijana kubadilisha mtazamo wa maaana ya Ajira kwa kutokukaa na kusubiri nafasi za ajira.

China na Marekani wapewa onyo

China ni moja ya nchi zinazodai kumiliki maeneo ya kusini mwa bahari ya China
Marekanai hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa bahari ya China, waziri wa ulinzi wa Merekani James Mattis ameonya.
Akiongea katika mkutano wa kiusalama huko Singapore, Bwana Mattis amesema kwamba hatua ya Uchina ya kutengeneza visiwa bandia na kuongeza uwepo wake wa kijeshi katika bahari ya kimataifa unahatarisha amani katika eneo hilo.
Hata hivyo amesema ugomvi kati ya Marekani na Uchina unaweza kuepukika, na akaipongeza Uchina kwa juhudi zake za kukabiliana na mgogoro unaotokana na uundaji wa zana za kinyuklia nhini Korea Kaskazini.
Matamshi hayo yanatolewa muda mfupi baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kuongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia majaribio kadha ya makombora mwaka huu.

Zidane: Ronaldo ni mchezaji bora

Kocha wa Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane amesema kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko alivyokuwa yeye enzi zake.
Zidane anatumaini Ronaldo ataiongoza Real kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo, itakapomenyana na Juventus ya Italia mjini Cardiff usiku wa Jumamosi.
Ronaldo amefunga jumla ya mabao 49 kwa klabu na nchi yake msimu huu na amefunga hat-tricks (mabao matatu katika mchezo mmoja) kwenye hatua zote, Robo Fainali na Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa.
Alipoulizwa katika mkutano na Waandishi wa Habaru, nani angekuwa bora kama wawili hao wangecheza zama moja, mshambuliaji gwiji wa Ufaransa Zidane, akasema: "Ronaldo, hakuna shaka.
"Anafunga mabao na hilo ndilo muhimu zaidi. Nilikuwa nacheza vizuri mno, lakini kufunga mabao siku mtu maalum. Nilikuwa mzuri katika kutengeneza nafasi za mabaoa. Nilifunga mabao fulani muhimu, lakini si megi kama yeye,'alisema.

Friday, 2 June 2017

ZILIZOMUBASHARA KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETINI JUMAMOSI JUNI 03 2017




Mwendokasi unasafirisha watu 200,000 kwa siku

. Mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) sasa unasafirisha watu 200,000 kwa siku kutoka watu 50,000 iliyokuwa ikisafirisha mwaka jana baada ya mradi huo kuanza kazi.
Kuongezeka kwa idadi hiyo inaelezwa kuwa ni ishara ya wananchi kuukubali mradi huo na kuutumia kila siku waendapo sehemu zao za kazi au majumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliotembelea mradi wa BRT, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka Dar es Salaam (DART), Hazina Mfinanga amesema mafanikio ya mradi huo yametokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya wadau mbalimbali.
Mfinanga amewataja wadau hao kuwa ni kampuni ya UdaRT ambayo ndiyo inaendesha mabasi, Maxcom Africa ambao wanaendesha mifumo ya kukusanya nauli na benki ya NMB ambayo inasimamia upatikanaji wa fedha za mradi huo.
"Bado tuko kwenye kipindi cha majaribio wakati tukiendelea na mchakato wa kupanua njia za BRT katika jiji hili ili watu wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huu," amesema Mfinanga.