Saturday, 1 April 2017

Wasiolipa kodi kinondoni wafungiwa maduka

Halmashauri ya manispa ya Kinondoni imeanza operesheni maalum ya kufunga maduka  ambayo yanaendesha shughuli zake bila ya kulipa kodi ambapo leo tayari imefunga maduka  zaidi ya tisini  na operesheni hiyo inaendelea katika maeneo yote ya manispaa hiyo lengo likiwa ni  kuhakikisha kila mtu analipa kodi kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Operesheni hiyo imefanywa afisa biashara wa manispaa hiyo Bw. Zahoro Haruna  kwa kuanzia katika eneo la makumbusho ambapo amesema watu wanadaiwa kodi na wamekuwa wagumu kulipa japo wamekuwa wakikumbushwa kila mara.
Baadhia ya waathirika wa opereshehi hiyo wamesema japo waliambiwa ila imewashuktukiza na hivyo wanaombaa kuongezewa muda ili waweze kujipanga vyema kwani kwa sasa biashara ni ngumu.

Meneja wa soko la Makumbusho Bw. Godfrey Makori  amewataka  wafanyabishara kutofanya biashara  kwa mazoea na sasa wajue nyakati zimebadilika  na hivyo walipe kodi za serikali.

No comments:

Post a Comment