Venezuela imetangaza kujiondoa kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa ya
Marekani Kusini OAS, ikidai mataifa ya jumuiya hiyo yanaingilia maswala
ya ndani ya Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bi Delcy Rodriguez ametoa kauli hiyo
punde tu baada ya kikao cha jumuiya hiyo ya OAS kupiga kura ya kuitisha
kikao maalum cha mawaziri wa mambo ya nje kujadili mzozo wa kisiasa
unaoendelea nchini humo.
Mataifa jirani ya Venezuela yameelezea wasiwasi wao kuhusu kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiuchumi inayoendelea nchini humo.
Wakati huohuo mtu mwengine tena amefariki huko mjini Caracas katika
maandamao ambayo yameikumba Venezuela kwa wiki ya tatu sasa
yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 30.
Mtu huyo alifariki baada ya kugongwa na bomu la kutoa machozi
lililorushwa na polisi waliokuwa wakijaribu kuwatawanya waandamanaji.
Waandamanaji hao wamekuwa wakimtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu kutokana
kuzorota kwa uchumi wa nchi hiyo jambo lililosababisha upungufu mkubwa
wa chakula.
No comments:
Post a Comment