Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata maelekezo kutoka kwa Mhandisi Mzawa baada ya kutembelea mradi huo.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na
wajumbe wa kamati ya mipango miji na kamati ya huduma ya jamii pamoja na
watendaji wa Halmshauri ya jiji wakati alipofanya ziara ya kutembelea
mradi wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na
maboresho ya maeneo ya umma katika fukwe ya Ocean Road.
wakandarasi wakiwa kwenye ujenzi
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akikagua mradi.
Mhandisi Mzawa akimuelekeza jambo Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wakipolikuwa kwenye eneo la mradi.
NA CHRISTINA MWAGALA,(OMJ) , Dar es Salaam.
Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa kuhimili athari
za mabadiliko ya tabia nchi pamoja na maboresho ya maeneo ya umma katika
fukwe ya Ocean Road.
Mradi huo ambao unatarajiwa
kumalizika Oktoba mwaka huu, utakuwa ni mahususi kwa wakazi wa jiji la
Dar es Salaam kwa ajili kutunza mazingira na kuepukana na mafuriko.
Alifafanua kwamba, mradi huo
utahusisha ujenzi wa vyoo na mabenchi ya kupumzikia, utakuwa na jumla ya
urefu wa mita 860 kuanzia Hospitali ya Agha-Khani kupitia viwanja vya
Ikulu.
“Ukiangalia kwenye fukwe zetu
hazina vyoo, hivyo kuwafanya watu wanaokuja kupumzika kukosa sehemu za
kwenda kujihifadhi, jambo ambalo sio zuri, ukizingatia jiji letu
linapokea wageni kutoka sehemu mbalimbali, ndio maana tumeamua kuleta
mradi huu ili kuondoa aibu hii” alifafanua.
Katika ziara hiyo iliyofanyika
hivi karibuni, Meya alisema kwamba maeneo ya kupumzikia katika jiji la
Dar es Salaam sio rafiki kutokana na ukosefu wa miundombinu hivyo
kukamilika kwa mradi huu kutaondoa baadhi ya changamoto zilizopo kwenye
maeneo ya hayo.
“Jiji letu ukiangalia
kimiundombinu haliko vizuri, mpangilio wake pia hauko vizuri, sasa
inapotokea mabadiliko yoyote, wananchi hujikuta kwenye athari kubwa
sana, hivyo kupitia mradi huu, utaondoa changamoto hizi” alisema Meya.
“ Ukienda kwenye majiji mengine,
utakuta sehemu za fukwe kama hizi , watu wanapumzika, lakini pia ni
chanzo cha mapato kwa jiji kwa sababu wanalipia, ila kwetu hapa, imekuwa
ni jambo la kawaida, watu wakuja kupumzika kiholela, huu ndio muda wetu
wa kulibadilisha jiji letu la Dar es Salaam” aliongeza.
Akizungumzia vikundi mbalimbali
ambavyo vilipewa mikopo kwa ajili ya kujiendeleza, Meya Isaya
alisisitiza kwamba, bado nafasi zipo kwa vikundi vingine vinavyohitaji
mikopo kwa masharti ya uaminifu.
Alifafanua kwamba vikundi vyote
ambavyo vitakidhi vigezo, vitapewa mikopo na kwamba lengo kubwa ni
kuwakwamua wananchi kiuchumi kupitia vikundi ambavyo vimeamua kujitoa
kwa ajili ya kupambana na umasikini.
No comments:
Post a Comment