Meya wa Jiji la Dar es
Salaam,Isaya Mwita akipunga mkono kuaga wananchi wake wa jiji lake
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar
es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya
kikazi ya siku kumi (10),akiwa nchini humo atakutana na Rais wa Iran,
Hassan Rouhani,Mwenyeji wake,Meya wa Jiji la Teheran, Muhammed Bakir
Galbaf na kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea nchini humo.
NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ
Meya wa jiji la Dar es Salaam
Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa mualiko wa ziara ya
kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili utakaofanyika
katika mji wa Bashar.
Aidha Meya atapata nafasi ya
kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan Rouhani kabla
ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar utakao
husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.
Katika mkutano huo ambao
utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada ya mkutano
huo ataelekea mjini Teherani kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo
Muhammed Bakir Galbaf ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa
za kibiashara katika majiji hayo mawilI.
Aidha katika mazungumzo hayo,
watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye majiji na
namna ambavyo wanaweza kuyatatua.
“ Iran na Tanzania ni nchi
marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi wamekuwa
wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji haya mawili
kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi
na wao wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.
Aliongeza kwamba akiwa nchini humo
atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu ambapo miongoni
mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni mmoja wapo.
“ Kushudia kwangu kampeni sio
kwamba nataka kugombea nafasi ya uras hapa nchini , hapana ila ni moja
ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao” alifafanua.
Hata hivyo Meya aliwasi wakazi wa
jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari
kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na mafuriko.
No comments:
Post a Comment