Saturday, 1 April 2017

Azam FC yatamba kuifunga Yanga leo

Baadhi ya wachezaji wa Azam FC wakipata maelekezo kutoka kwa mwalimu wao.
Kocha Mkuu wa AzamFC, Aristica Cioaba ameweka wazi kuwa hana presha yoyote kuelekea mchezo unaopigwa leo dhidi mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga anadai kwa kikosi chake leo anaamini kitaibuka na ushindi tu dhidi ya mabingwa watetezi
Mtanange huo utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni, ambapo Azam FC ina morali kubwa kuelekea mtanange huo huku ikiwa imepanga kuendeleza wimbi lake la matokeo mazuri kwenye mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
“Naiheshimu Yanga ni timu kubwa hapa Tanzania, msimu uliopita walikuwa mabingwa wa ligi hapa Tanzania, naijua vilivyo Yanga, nawaamini vijana sana wataingia uwanjani na kusahau mechi iliyopita ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuanza upya kwa kucheza vizuri na kupata matokeo. Umeona Azam FC katika miezi mitatu hii, imecheza mechi zake zote kwa nguvu na kukusanya pointi nyingi,

imepoteza mchezo mmoja tu ambao ni wa Kombe la Shirikisho Afrika, nadhani kila mmoja hapa anatambua mechi kubwa dhidi ya Simba na Yanga, na mimi umakini wangu ni kuwaweka vema wachezaji ili kuwa na moja ya matokeo mazuri, nahitaji kucheza mchezo mzuri na kushinda mechi ya leo,” alisema Cioaba

No comments:

Post a Comment