Na Jimmy Mengele – Dodoma.
Mfuko wa Pensheni wa PPF
unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na PPF ili kuweza kufaidika na
fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo, elimu, huduma ya afya,
mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.
Akiongea katika Maonesho ya
uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma,
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel alisema hii ni fursa
pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu, madaktari na kada zingine
kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya
kimaendeleo.
Afisa huyo alisema waajiriwa hao
wapya wakijiunga na PPF watafaidika na mikopo katika maeneo yao ya kazi,
mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya ugonjwa, mafao ya kifo,
wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wakati kwa
kutumia kikotoo kilichoboreshwa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi,Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akisaini kitabu cha wageni
katika banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi baada ya kupata maelezo ya mpango wa ‘ Wote scheme’ ambao
umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana kutokana na mikopo ya
mpango huo, waliosimama Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel
na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF
Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga wakitoa maelezo juu
ya huduma za PPF kwa Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe.
Charles Mwijage wakati alipotembelea Maonesho ya Mifuko ya uwekezaji
kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
Afisa Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya
Mashariki na Kati Joyce Rwechungura akitoa maelezo ya kazi mbalimbali
zinazofanywa na PPF kwa waliotembelea banda la PPF katika Maonesho ya
Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inayoendelea katika viwanja vya
Mashujaa mkoni Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Kishetu Mhe.
Elias Kwandikwa akiuliza swali juu mpango wa ‘Wote scheme’
ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta isiyo rasmi nao
kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali. Wanaomfuatilia kwa makini ni
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF
Astro Liganga.
Katibu wa Chama cha Wafugaji
Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa PPF
Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao kima cha chini cha
kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani yake kuna fursa za mikopo
ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo
huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.
Michael Silasi (mwenye miwani ) na
Said Ally (aliyevaa kofia ) wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
PPF Janet Ezekiel kuhusu kazi za PPF na mafao yanayotolewa na Mfuko huo
ikiwemo mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao utoa fursa za mikopo ya maendeleo,
mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu
unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.
No comments:
Post a Comment