Tuesday, 25 April 2017

Kupitia ukurasa wa Haji Manara ameandika haya

Mkuu wa  Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amefunguka mapya huku akidai yeye siyo mtu anayeamini uonevu na wala siyo mtu ambaye anaweza kunyamaza akiona haki yake inaporwa.
Manara amesema hayo kupitia ukurasa wa kijamii Istagram alfajiri ya kuamkia leo huku akilalama kuwa ‘Natural justice’ katika nchi hii haitambuliki kwa kuwa hakupatiwa nafasi ya kusikilizwa upande wake binafsi kabla ya kupewa hukumu.
“Natural justice nchi hii haitambuliki! wahaini na wauaji nao pia husikilizwa, iweje kwa mtuhumiwa ambaye anapigia kelele haki ya mwajiri wake?.....Ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu ila nawaambia TFF Haji  Manara hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili lakini nina moyo wa simba nitapambana kwa kiwango cha juu sana”. Ameandika Manara
Vile vile Manara amesema atadai haki yake pamoja na mwajiri wake kwa viwango huku akiziomba kamati za Shirikisho za Soka Tanzania (TFF) zipokee rufaa yake .

“Nitaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa, nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki”. Alisisitiza Manara

No comments:

Post a Comment