Mbeya City Yapata Mdhamini Wa Vifaa Vya Michezo
Mfano wa Vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na Timu ya Mbeya City kuanzia msimu ujao.
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Mussa Mapunda akisaini mkataba wa
makubalino na uongozi wa Kampuni ya Sports Master chini yake Fadhili
Nsemwa (kulia).
Mwenyekiti wa Timu ya Mbeya City, Mussa Mapunda (kushoto) akipokea
mkataba kutoka kwa Kiongozi wa Sports Master ambao ni wadhamini wapya
watakaosimamia maswala yote ya vifaa vya michezo vya Timu hiyo, Fadhili
Nsemwa, baada ya kusainiana makubaliano.
Timu ya soka ya Mbeya City imepata mfadhili mpya wa timu hiyo ambaye
atakuwa anasimamia maswala yote ya vifaa vya michezo ikiwemo jezi zote
za timu hiyo zitakazotumiwa na wachezaji na zile za mashabiki kuanzia
mwezi wa saba mwaka huu. Viongozi hao wamesaini mkataba wa udhamini huo
uliofanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya Mbeya Hill View kwa
kuwaalika wadau wa mbeya city na vyombo vyote vya habari.
No comments:
Post a Comment