Waziri wa Afya, Maendeleo ya
jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa
Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa
Masuala ya Usawa wakijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE)
jijini Dar Es salaam.
Prof Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu
wa Chuo kikuu cha Dar Es Salaam akihutubia wadau na wanafunzi
waliojitokeza katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Jinsia na Usawa
yaliyofanyika katika chuo kikuu cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof.
William Anangisye akihutubia jopo la Wadau na wanafunzi katika mkutano
wa masuala ya Usawa na huku akisisitiza wazazi na walezi kuwatia moyo
wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kupata wanasayansi
wanawake nchini.
Wadau wa Masuala ya Usawa wa
kijinsia wakifuatilia kwa ukaribu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Mh.Ummy
Mwalimu Waziri wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na
watoto aliyekuwa akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan
katika viunga vya Chuo cha Uwalimu DUCE jijini Dar Es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa
masuala ya Usawa wakijinsia katika mkutano wa kwanza wa masuala ya Usawa
wakijinsia uliowakutanisha kujadili na kuhamasisha juu ya kumlinda
mtoto wa kike ili apate Elimu sawa kama ile apatayo mtoto wakiume katika
jamii yetu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa
wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo
yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha
Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano
waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.
“Tunapokataza watoto wa kike
wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni
tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa
wakati waliotarajia”alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
anaunga mkono uamuzi wa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike
kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.
Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa
wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya
sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na
viwanda nchini.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha
DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la
mkutano huo ni
kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda masomo ya
sayansi ili kupata wanasayansi wanawake nchini.
No comments:
Post a Comment