Sunday, 30 April 2017

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe hazipandisha hoteli za Dar kuwa za nyota tano

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi za Hotel zilizopo jijini Dar es Salaam na kwa kuzipa madaraja mpaka nyota tano  katika soko la utali hapa nchin, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe  akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa  Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli, Seraphin Lusala baada ya Hoteli hiyo kutambuliwa kuwa na hadhi ya Nyota tano katika mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

  Majaji ambao waliokuwa wakitoa maksi ya hadhi za hoteli hapa nchini wakisimama kujitambulisha kwa wageni waliofika.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi akizungumza na Wamiliki wa Mhoteli jijini Dar es Salaam leo kabla ya kukabidhi vyeti vya madaraja ya hotel zao.

 Afisa utalii kutoka bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Irene Mville akitoa maelekezo kwa wadau wa mahoteli ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa madarajana viwango katika Hoteli zilizopo jijini Dar es Salaam .

 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Hotel jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment