Sunday, 30 April 2017

Nape:Heshima ya binadamu na maana ya kweli ya ubinadamu ni kutokaa kimya pale uovu unapotendeka


Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye amemkumbuka marehemu baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuamua kutumia maneno yake katika kufikisha ujumbe wake kwa wananchi kupitia ukurasa wake wa twitter 

Mhe Nape Nnauye alikuwa akitoa ujumbe kuwa maana ya ubinadamu na heshima ya binadamu ni kutokaa kimya pale jambo la uovu linapokuwa likitokea, akiwataka wananchi kutokaa kimya wanapoona kuna jambo la uovu linatendeka.
Ili kufikisha ujumbe huo vizuri Mhe. Nape Nnauye ilibidi atumie clip ya video ya marehemu baba wa taifa, Julius Kambarage Nyerere wakati akihotubia kwa mara ya mwisho katika Mkutano Mkuu. Ambapo mwalimu alisema maneno haya kwa lugha ya kiingereza  
"Hotuba yangu ya mwisho kwenye huu mkutano mkuu, nimeelezea matukio na mienendo na mahitaji kwa namna ambavyo sisi Watanzania tuonavyo, kukaa kimya pale tuonapo hatari, kutulia tu pale tuonapo sera hatari ambazo ziko kinyume na kulinda amani na haki, kufanya hivyo itakuwa tunaachia uhuru wetu na utu wetu kamwe hatutafanya hivyo" Mwalimu Nyerere 

Baada ya kuweka video hiyo ya Mwalimu Nyerere Nape Nnauye naye aliweka ujumbe wake ambao ulisomeka hivi 

"Heshima ya binadamu na maana ya kweli ya ubinadamu ni kutokaa kimya pale uovu unapotendeka" aliandika Nape Nnauye  

No comments:

Post a Comment