Saturday, 29 April 2017

Asali inavyoweza kutibu magonjwa mbalimbali

Huko Misri kuligunduliwa mwili wa mtoto ambao haukuoza katika mojawapo ya wafalme wa zamani ,mwili huo ulikuwa umetiwa ndani ya chombo kilichojazwa asali.Tukio hili laonyesha kuwa asali ina siri kubwa iliofanya mwili wa mtoto huyu kutooza tangu miaka 4500 iliyopita.

Image may contain: candles 1.Kujikuna
Tia asali ndani ya kikombe na kisha ongeza vaselini na mafuta waridi jipake mahala panapowasha asubuhi na jioni,na jiepushe na vinavyochochea kujikuna.
2.Uzuri wa uso
Upake asali uso wote wakati mwili upo katika mapumziko baada ya robo saa osha uso kwa maji ya vuguvugu na kausha,halafu jipake kidogo mafuta ya zaituni.Endelea kufanya hivi kwa muda wa wiki moja mfululizo.
3.Jeraha(kidonda)
Paka asali penye kidonda na funga bandeji na uepushe umajimaji,usifungue mpaka baada ya siku tatu.
4.Kuungua
Chukua asali na uchanganye na vaselini kiasi kama kama hicho cha asali halafu jipake mahala palipoungua asubuhi na jioni mpaka ile ngozi iliyoungua ibanduke.Au changanya yai katika asali kiasi cha kijiko kimoja na jipake mahala palipoungua kila siku.
5.Kuua chawa na mayai yake
Paka kichwa chote asali pamoja na kukisugua vizuri mpaka uhakikishe kuwa  imeingia vema hadi mashinani halafu jifunge kitambaa iwe kabla ya kulala.Asubuhi osha kwa maji ya uvuguvugu pamoja na kuchana nywele .Endelea namna hii kwa muda wa wiki moja mfululizo.
6.Kukosa usingizi
Chukua glasi ya maziwa na changanya na asali kijiko kikubwa na unywe kabla ya kulala.
7.Maradhi ya kinafsi na wazimu
Mgonjwa ale asali na mgongo wake uumwe na nyuki,na pale alipoumwa apake asali.Aendelee hivyo japo kila mwezi mara moja na aendelee kula asali,kutafuna nta yake na nyuma ya kichwa chake apake sega la nyuki kidogo.
8.Kifafa
Asubuhi kabla ya kunywa chai,anywe asali kikombe kimoja na jioni kikombe kimoja.Aendelee hivyo kwa wiki moja.
9.Magonjwa yote ya macho
Jipake asali asubuhi kama vile unapaka wanja,vilevile kabla ya kulala pamoja na kunywa asali kijiko kimoja.
10.Kiungulia/Asidi
Meza punje ya kitunguu saumu kabla ya kula meza na kikombe cha maziwa yaliyochanganywa asali kijiko kimoja kwa muda wa siku tano.
11.Kuhara/Tumbo la kuendesha
12.Kufunga choo
Kufunga choo ni kinyume cha kuharisha.Chukua maziwa baridi kikombe kimoja korogea asali ndani yake kijiko kimoja halafu unywe,fanya hivyo asubuhi na jioni.
13.Kutapika
Chemsha karafuu na korogea asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja kabla ya kula chakula;kutapika na kichefuchefu kutaisha.
14.Kidonda
Chukua asali nusu kikombe na kikombe cha maziwa na changanya unga wa ganda la ndizi lililokaushwa kijiko kimoja,Tumia asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi
15.Maradhi ya kifua
Chukua juisi ya figili kikombe kimoja na korogea asali kijiko kimoja.Kunywa asubuhi na jioni.Vilevile unaweza kuchukua ubani dume ukautia ndani ya maji na kuchanganya na asali kijiko kimoja ili kuyapa mapafu nguvu.
16.Harufu mbaya mdomoni
Chukua asali vijiko viwili ikoroge ndani ya maji na kisha chemsha katika moto mdogo mpaka itoe moshi. Vuta puani na mdomoni moshi huo kupitia kwenye paipu au bomba lililofungwa vizuri katika chombo.Endelea na tiba hii pamoja na kutafuna nta ya asali.
17.Kukaukiwa na sauti
Fany kama dawa hiyo iliyotangulia (harufu mbaya)pamoja na kugogomoa asali na chumvi kidogo kwa muda wa siku tatu.
18.Homa ya mafua(Influenza)
Vuta puani moshi wa kiziduo cha asali na kitunguu maji kabla ya kulala pamoja na kunywa asali kijiko kimoja baada ya chakula.Tiba hii hufanywa kwa kuchukua asali na kitunguu maji kidogo kilicho chambuliwa maganda;vikatiwa katika chombo chenye maji na kuchemsha juu ya moto mdogo hadi moshi utoke.
19.Malengelenge ngozini



Chukua binzari nyembamba kiasi cha kikombe na changanya na asali nusu kikombe kisha chemsha pamoja na kuhifadhi ndani ya chupa safi halafu uwe ukijipaka.
20.Maumivu ya fizi na kuyapa meno nguvu
Changanya asali na siki na usukutue asubuhi na jioni.Vilevile waweza kusugua fizi kwa asali;sugulia kwa mswaki(asali iwe ndio dawa ya mswaki)dawa hii hukinga meno yasioze na huyapa meno na fizi nguvu.
21.Mishipa iliyovimba
Kwa maradhi yote ya ugonjwa huo pamoja na vidonda tumia asali kama mafuta ya kujipaka mara tatu kwa siku.Jipake taratibu na kunywa asali kijiko kimoja kila umalizapo kula.Endelea hivyo mpaka utakapopona.
22.Kidonda kilichooza
Chukua asali kikombe kimoja na mafuta ya ini la samaki kikombe kimoja yachanganye pamoja na ujipake baada ya kusafisha kidonda kwa asali iliyochanganywa na maji ya moto.Fanya hivyo kila siku hadi upone.
23.Kidonda kisichopona
Tumia gundi ya asali kwa maradhi haya.Jifunge bandeji kwa gundi hiyo pamoja na kukisafisha kila siku na kubadilisha bandeji,pamoja na kunywa asali kijiko kimoja asubuhi na jioni kabla ya kula chakula.
24.Kifua kikuu na mapafu
Changanya maji ya waridi na asali vipimo sawa  alafu kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni na ujipake kifuani na shingoni .Mafuta ya zaituni yaliyopigwa kwenye asali jipake kabla ya kulala.Endelea hivyo mpaka upone.
25.Uvimbe wa tishu za msuli kwenye moyo na kutetemeka
Changanya asali vijiko viwili ndani ya maji ya baridi glasi moja kisha unywe kabla ya kula chakula .
26.Moyo kubana
Kila baada ya kula kunywa asali kijiko kimoja ikifatiwa na juisi ya karoti.Fanya hivyo kwa muda wa mwezi mmoja
27.Uvimbe mdomoni na ulimi kufura
Tia kijiko cha asali ndani ya nusu kikombe cha maji ya moto na sukutua mara tatu kwa siku kila siku.
28.Maradhi ya masikio na maumivu
Changanya asali katika maji na chumvi kidogo na utie sikioni matone kidogo kabla ya kulala kila siku.
29.Baridi yabisi(Rheumatism)
Kunywa asali iliyochanganywa na maji na mafuta ya habatsouda(maji yawe ya uvuguvugu).Pia jipake mafuta ya habatsouda yaliyochanganywa na mafuta ya kafur na mafuta ya zaituni na asali kwa vipimo sawa;Jipake kabla ya kulala na jifunge kitambaa cha sufi mahali panapouma.Pia kuumwa na nyuki penye maumivu hutibu baridi yabisi,baada ya hapo paka asali mahali palipoumwa.
30.Jongo(Edema)
Kunywa mchanganyiko wa asali na ubani dume asubuhi na jioni.
31.Sugu/Chunju
Chukua gundi ya nyuki upashe moto na kuweka juu ya sugu na ufunge vizuri kisha acha kwa siku tatu mpaka sugu iondoke.
32.Magonjwa ya ini
Chukua ganda la muoka (mualoni)lisage vizuri,chukua kiasi cha kijiko kimoja ukoroge katika asali na uwe ukila kabla ya kula chakula kwa muda wa mwezi mmoja.
33.Kutia nguvu na nishati
Chemsha majani ya chai halafu uyachuje na kuchanganya na asali.Kunywa kama chai kila siku.
34.Maradhi ya wanawake na uzazi
Kunywa kikombe kimoja cha asali kwa mama anayesikia uchungu wa kuzaa humsaidia kuzaa kwa urahisi.Baada ya kuzaa mzazi ale kwa wingi mkate wa ngano asili na asali.Kwa anayetaka hedhi imtoke na pia kumaliza maumivu yake Chemsha uwatu kiasi cha kikombe kimoja,ongeza asali na anywe kila siku asubuhi na jioni.Pia inashauriwa mwanamke kusafisha uke kwa asali na maji ya moto ili kumpatia nafuu,badala ya kwenda kusafishwa na vifaa vinavyo muumiza na kumdhuru.
35.Nguvu za kiume
Chukua vitunguu maji vitatu viponde na kuvikamua vizuri maji yake kisha changanya na asali kiasi hichohicho cha maji ya vitunguu na ubandike juu ya moto mdogo huku ukikoroga mpaka povu la asali limalizike halafu tia ndani ya chupa.Kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula kila siku.Waweza pia kuiboresha kwa kuongeza habatsouda na figili iwe kama jam (marhamu).
36.Utasa/ugumba
Kula mkate wa nyuki ulio mpya yaani baada ya kutolewa kwenye mzinga na baadae kunywa maziwa ya ng'ombe glasi moja yaliyochanganywa na unga wa pembe ya kifaru miligram tatu.Fanya hivyo kwa mda wa mwezi mmoja.
37.Saratani
Chukua mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligram miamoja kula kila wiki mara moja ikifatiwa na kula asali pomoja na nta yake kila siku kiasi cha kikombe kimoja na sugua mwili wako kwa asali na mafuta ya habatsouda kisha oga baada ya lisaa limoja kwa maji ya vuguvugu na baadae kula asali iliyochanganywa na unga wa habatsouda katika juisi ya karoti kila siku.
38.Ukoma
Changanya asali na amonia na jipake kila siku hadi upone.
39.Kinga ya sumu
Chukua mafuta ya ufuta (simsim)kiasi cha kijiko kimoja changanya kwenye kikombe cha asali na uwe unakunywa kila asubuhi na jioni kunywa asali iliyochanganywa kwenye kikombe cha maziwa ya moto na ambari kidogo endekea hivyo kila siku kwa muda wa siku tatu pamoja na kutokula nyama.
40.Tezikibofu
Kula mkate wa nyuki kutoka mzingani moja kwa moja kiasi cha miligram hamsini kisha oga na maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na asali wakati wa jioni.

No comments:

Post a Comment