Friday, 28 April 2017
Polisi waizuia CUF upande Maalim Seif.kufanya Usafi
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, imepiga marufuku usafi ulipangwa kufanywa na Chama cha Wananchi CUF upande maalim seif.
Hayo yamekuja baada ya Wanachama wa CUF zaidi ya elfu tano na wabunge wa CUF 42 ambao wanamuunga mkono Maalim Seif kupanga kwenda kusafisha ofisi ya chama chao CUF Makao Makuu Buguruni siku ya Jumapili ya tarehe 30 mwezi huu wa nne.
Akiongea na waandishi wa habari Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea akiwa ameambatana na wabunge wengine 41 amesema wameamua kufanya usafi katika ofisi ya chama chao baada ya kuona ofisi hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na Profesa Lipumba na genge lake kufanya mipango ya kuvamia mikutano ya watu, na matukio ya kihalifu.
"Siku ya Jumapili ya tarehe 30 mwezi wa nne mwaka huu, wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambao hawamkubali Professa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti wa CUF wameamua kwenda kufanya usafi kwenye ofisi zao za Buguruni ofisi kuu za chama, hatua hii imekuja baada ya kuona ofisi ile inatumika vibaya kimekuwa ndiyo kijiwe cha wahuni kupanga matukio ya kihalifu kwenda kuvamia mikutano, kuvamia watu sisi kama wanachama tumesema hapana hatuwezi kuacha ofisi yetu itumike vibaya hivyo" alisema Mtolea
Mbali na hilo Mtolea amesema wazo hilo lilianzia Temeke lakini limepokewa vyema na sehemu zingine hivyo baadhi ya wanachama kutoka Zanzibar, Tanga na wanachama wa maeneo jirani wataunga na wabunge 42 kufanya usafi huo hapo Buguruni.
"Wazo limeungwa mkono na wanachama wote wa jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani hivyo wanachama kutoka Mkuranga, Kibiti, kutoka Rufiji, Bagamoyo, Kisarawe, kutoka Kibaha na wenyewe wamesema kuwa watakuja lakini hata nje ya maeneo hayo kama wanachama kutoka Tanga mjini, Babati, Kondoa, kutoka Zanzibar na wenyewe pia wamesema wamehamasika kufanya usafi huo hapo Buguni, kwa hiyo tunatarajia zaidi ya wanachama elfu tano watajitokeza Buguruni kwa ajili ya kuisafisha ofisi yao" alisisitiza Mtolea
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment