Sunday, 30 April 2017

Manuwari za China zatia nanga Ufilipino

Manuwari za Uchina zimewasili Ufilipino kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba huku Ufilipino ikiimarisha uhusiano wake na Uchina.
Manuwari hizo tatu zilitia nanga mjini Davao.
Ziara hiyo inafanywa siku moja baada ya mkutano wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ambao ulifanywa Ufilipino ambapo malalamiko dhidi ya harakati za Uchini katika Bahari ya Kusini ya Uchina, hazikuzungumzwa sana.

Kabla ya Rodrigo Duterte kuwa rais wa Ufilipino, nchi hiyo ikilalamika vikali juu ya hatua za Uchina katika bahari hiyo.

No comments:

Post a Comment