Mkurugenzi wa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekanusha kuwepo kwa taarifa
zinazotoa tahadhari dhidi ya matumizi ya mafuta ya alizeti kutokana na
mbegu za alizeti kuchafuliwa na sumukuvu tahadhari iliyotokana na
utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha MarekaniAkizungumza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kutokana na utafiti uliofanyika na wataalam kwa kutumia mashudu na mbegu za alizeti utafiti huo hautoshelezi kuthibitisha kuwepo kwa sumu hiyo ambayo ni hatari kwa walaji.
Bw. Sillo amesema kuwa wananchi waendelee kuyatumia mafuta hayo hasa yaliyothibitishwa na mamlaka hiyo bila wasiwasi na kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na taarifa ya utafiti huo.
No comments:
Post a Comment