WADAU wa Sekta binafsi nchini
Jumanne wiki hii, wamefanya mkutano ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mkutano wao na serikali chini ya jukwaa la Baraza la Taifa la Biashara
(TNBC) unaotarajiwa kufanyika Mei 6 mwaka huu.
Mkutano huo wa ndani uliandaliwa
na Taasisi ya Sekta binafsi nchini – TPSF ulilenga kuwekana sawa kuhusu
namna bora ya kuiwakilisha sekta binafsi katika mkutano huo muhimu,
ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli.
Akiwakaribisha wadau wa Sekta
Binafsi katika kikao hicho cha maandalizi Mwenyekiti wa TPSF Dk.
Reginald Mengi alisema Serikali na Sekta Binafsi hawakomoani, ndio maana
TPSF inahimiza wafanye kazi kwa pamoja ili kulifikisha taifa kwenye
uchumi wa viwanda.
Dk Mengi pia alisema serikali na
sekta binafsi wana malengo yanayofanana ya kutokomeza umaskini na
kutengeneza ajira kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kutekelezeka kwa
urahisi iwapo kutakuwa na ushirikiano wa karibu baina ya serikali na
Sekta Binafsi.
Katibu Mtendaji wa TNBC Mhandisi
Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo utakuwa ni fursa nzuri kwa serikali
na sekta binafsi kubadilishana mawazo kuhusu wajibu wa kila upande
katika kuboresha mazingira ya biashara na uzalishaji nchini ili kukuza
uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment