Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya
Malaria Duniani kwa waandishi wa Habari Mjini Dodoma na kusisitiza kuwa
vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni bure kwa vituo vyote vya Afya
vya Umma nchini.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu
cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya
Malaria Duniani.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na
Wawakilishi kutoka kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua
Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku
ya Malaria Duniani.
Picha zote na Raymond Mushumbusi Dodoma MAELEZO.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haitosita
kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya Umma
nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo vya
malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati
akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria
Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima
malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya
Umma.
“Huduma ya kupima Malaria na dawa
za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma vya Huduma
za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka kutekeleza
agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.
Aidha amwewaagiza Waganga wakuu wa
Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa karibu ili
kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.
Mhe Ummy Mwalimu amewashukuru
wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio yaliyofikiwa
ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.
Siku ya Malaria Duniani
uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni “
Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.
No comments:
Post a Comment