Aliyekuwa katibu mkuu wa klabu ya
Simba,Mwina Kaduguda amesema kwamba kwa sasa mpira wa miguu hapa nchini
unaendeshwa na watu wasio na uelewa wa mchezo huo ndio maana mara kwa
mara kunaibuka migogoro ambayo haina msingi.
Kaduguda ameshangazwa na
yanayoendelea hivi sasa juu ya sakata la mchezaji wa timu ya Kagera
Sugar Mohamed Fakh aliyecheza mechi zidi ya Simba akiwa na kadi tatu za
njano baada ya kubainika na kamati ya masaa 72.
Hata hivyo alisema kwamba
migogoro hiyo haitaweza kuisha endapo kama viongozi wanaongoza mpira
wataendelea kuwa walewale wa siku zote ambao kiuhalisia hawana hadhi ya
kuongoza mpira wa miguu.
No comments:
Post a Comment