Rais John Magufuli amesema kati ya madaktari 500 walioonyesha nia ya
kwenda kufanya kazi nchini Kenya watachaguliwa 258 na kuajiriwa na
serikali ya Tanzania mara moja kuanzia sasa.
Taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ilieleza kuwa
hatua hiyo imefuatia baada ya kutetereka kwa makubalino ya serikali ya
Tanzania na Kenya baada ya Mahakama nchini Kenya kutoondoa pingamizi
lililofunguliwa kuhusu ajira za madaktari wa Tanzania nchini humo.
“Rais Magufuli ameamua kuwa, madaktari hao 258 ambao walikuwa tayari
kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na serikalini mara moja.
Kufuatia uamuzi huu, majina ya madaktari husika na vituo
watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya wizara
www.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta
maombi yao na kukidhi vigezo,” amesema Ummy.

No comments:
Post a Comment